TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

GEITA INAFANYA VIZURI MAPAMBANO DHIDI YA TB & HIV.

Dr Godluck Lyatuu, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la MDH hapa nchini. 

Na Urban Epimark, Geita.


Imeelezwa kwamba mkoa wa Geita unafanya vizuri katika mradi wa Afya Jumuishi unaotekelezwa na Shirika la MDH kwa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya TB na HIV.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la MDH Dr Godluck Lyatuu katika mkutano wa siku mbili wa timu ya mkoa wa Geita wa kutathmini mafanikio ya utekelezaji ya nusu mwaka wa mradi wa Afya Jumuishi unaotekelezwa na MDH uliofanyika mjini Geita Mei 25 & 26 mwaka huu.


"Natumia nafasi hii kuipongeza sana timu ya utekelezaji mradi wa Afya Jumuishi ya mkoa wa Geita kwa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya TB & HIV katika kipindi cha utekelezaji cha nusu mwaka"  alisema Mkurugenzi wa Miradi.


Kulingana na taarifa zilizowasilishwa katika mkutano huo na wakuu wa vitengo vya TB, HIV na uchanjaji wa UVIKO-19 takwimu zinaonesha mafanikio ni mazuri na ya kutia matumaini kwani malengo ya utoaji huduma yaliyopangwa yamefikiwa katika Halmashauri zote na nyingine kuvuka katika mkoa wa Geita.

 


Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita- (Acting RMO Geita) Dr Amos Jeremiah akiongea katika mkutano huo. 

Pia imeelezwa mbali na changamoto chache zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mpango wa mradi, mkoa wa Geita umefanikiwa kushika nafasi ya nne kitaifa dhidi ya mikoa yote nchini katika kukusanya na kuwasilisha sampuli za damu kwa ajili ya vipimo kwa wakati kwenda makao makuu ya upimaji TB & HIV jijini Dar es Salaam. 


"Timu ya Afya ya Jamii ya mkoa wa Geita, tembeeni vifua mbele kwani mkoa wetu kwa sasa ni wa nne kitaifa dhidi ya mikoa yote nchini katika kukusanya na kuwasilisha sampuli za damu kwenda kwenye vipimo Dar es Salaam" mkutano huo uliambiwa na Dr Furaha Kibaba ambae ni  Mratibu wa shughuli za maambukizi ya Virusi vya Ukwimu katika mkoa wa Geita.


Nalo Shirika la MDH hapa nchini linalotekeleza mradi huo wa Afya Jumuishi katika mkoa wa Geita, uongozi wake wa juu kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam umefanya mabadiliko ya safu ya uongozi katika mkoa wa Geita.

 


Dr Furaha Kibaba ambae ni Mratibu wa shughuli za kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa Geita (RACC) akielezea mafanikio yaliyofikiwa. 


Aliyekuwa Meneja wa Mradi katika mkoa wa Geita (RPM) Dr Emanuel Sima (pichani) amepandishwa cheo na kuhamishiwa Makao Makuu ya MDH jijini Dar es Salaam kwenda kuwa Meneja Mwandamizi wa Huduma za Afya ya Jamii (Senior  Community Services Manager) kuanzia sasa.


Dr Sima ambae alijiunga na Shirika la MDH mwaka 2018 na kuhudumu katika nafasi mbalimbali katika mkoa wa Geita na kisha baadae kuwa Meneja wa Mradi, amefanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa kutokana na juhudi na uwezo binafsi na uchapazi kazivwake ulio mzuri hadi sasa anaondoka akiuacha mradi ukiwa katika viwango vizuri vya mafanikio.


Akitoa neno la Shukrani kwa ushirikiano alioupata kwa watumishi wa MDH Mkoa wa Geita Dr Sima aliwataka kuendelea kuwa wamoja na wabakie katika mtizamoa mmoja muda wote (Don’t lose Focus) na watakutana katika majukumu ya kazi endapo atakuja mkoani Geita baadae.

 


Washiriki wa mkutano huo timu ya mkoa wa Geita katika mradi wa Afya Jumuishi unaotekelezwa na Shirika la MDH wakiwa katika mkutano huo mjini Geita uliofanyika Mei 25 & 26, 2022 

Nafasi yake kwa sasa inachukuliwa na Dr Nicolous Tarimo (pichani) ambae kitaaluma pia ni Daktari wa Binadamu.


Dr Tarimo alijiunga na timu ya MDH mkoa wa Geita mwaka jana 2021 mwezi August, akitokea mkoa wa Kagera.


Mkutano huo ulipokea taarifa za mabadiliko hayo ya uongozi wa juu wa MDH ngazi ya mkoa wa Geita, na kuwatakia mafanikio mema Dr Sima na Dr Tarimo katika majukumu yao mapya.

 


Dr Emanuel Sima (pichani) ambae alikuwa Meneja Mradi wa Shirika la MDH mkoa wa Geita (RPM) amehamishiwa MDH Makao Makuu Dar es Salaam kuwa Meneja Mwandamizi wa Huduma za Afya kwa Jamii (Senior Community Services Manager) 



Dr Nicolous Tarimo (pichani shati jeupe) ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Mradi wa MDH katika Mkoa wa Geita (RPM) kuchukua nafasi ya Dr Emanuel Sima anae hamia MDH Makao Makuu. 



Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la MDH hapa nchini Dr Godluck Lyatuu (katikati shati la draft) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa nusu mwaka wa kutathmini mafanikio ya mradi wa Afya Jumuishi unaotekelezwa na MDH mara baada kumalizika kwa mkutano huo mjini Geita Mei 26, 2022


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments