Na Urban Epimark, DAR ES SALAAM
Msajili wa Hazina Bw Neemia Mchechu ameya taadharisha mashirika ya umma nchini kuwajibika ipasavyo kwa kumwelewa vizuri Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anavyo taka kuhusu uwekezaji nchini na kuwataka wawe wasikivu wazuri katika kupokea maoni ya wadau ili kuboresha na kuvutia uwekezaji nchini.
Bw Mchechu ameyasema hayo kwenye mkutano wa wadau wa usafirishaji mizigo kwa njia ya anga ulio andaliwa na Shirika la Ndege nchini ATCL ulifanyika jijini Dar es Salaam March 20, 2023.
"Ofisi ya Msajili wa Hazina ndio inayo simamia mashirika yote nchini hivyo ni vizuri mashirika ya umma yakamwelewa vizuri Rais Dkt Samia kuhusu uwekezaji unao utaka nchini hususani kwa kusikiliza vizuri maoni na ushauri unao tolewa na wadau wa uwekezaji ili boresha mazingira ya kuvutia uwekezaji zaidi kutoka nje" alieleza Msajili.
Bw Mchechu ambae ndie alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo uliojumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji mizogo kwa njia ya anga ulio andaliwa na ATCL alisema, ili uwekezaji ufanye vizuri zaidi nchini, sekta ya umma inabidi kwenda na kasi ya Sekta Binafsi ili mambo yaende sawa.
Amezishauri taasisi mbalimbali za umma zinazo wajibika kwenye mlolongo wa uwekezaji pamoja na upande wa kodi kuwajibika zaidi na kuwa radhi muda wote kusikiliza maoni ya wadau ili kuondoa baadhi ya vikwazo katika kutanua uwekezaji zaidi nchini.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya usafirishaji mizigo kwa njia ya Anga ya Swissport Tanzania Bw Mrisho Yassin ameishauri Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwa "flexible" katika kusimamia sheria za kodi husani kwenye mpango wa ushirikiano wa kiubia kati ya sekta ya Umma na Binafsi nchini yaani "Public Private Partinaship-PPP"
Bw Yassin aliilalamikia TRA inavyoibana Swissport Tanzania katika kufanya uwekezaji zaidi kwenye miundo mbinu inayo husisha umiliki wa ardhi na kusema, Swissport inashindwa kuwekeza zaidi nchini kutokana na muundo wa sheria hiyo ya "Public Private Partinaship" ambapo wao hawamiliki ardhi hapa nchini.
Mwisho.
0 Comments