Na Victor Bariety;
Muda unazunguka, saa za siasa
zinahesabu sekunde zake, na Arumeru Magharibi iko kwenye moto wa matumaini.
Kila kijiji, kila mlima, kila
daladala ina jina moja linalotamkwa kwa sauti ya shauku Dkt. Johannes
Lembulung Lukumay, au kwa jina walilomtunuku wananchi wake:
Komando wa Maendeleo.
Huyu ni zaidi ya mgombea. Ni daktari aliyegeuka kuwa nguzo ya matumaini, mwanadamu mwenye utulivu wa kipekee, anayepigana vita isiyo na risasi vita ya umasikini, ujinga na kukata tamaa.
Kwa macho ya wengi, hizi ni siku za
mwisho za kusubiri. Siku za Komando kuikomboa Arumeru zahesabika.
Uungwana Unaovuta Uongozi
Dkt. Lukumay anatembea bila majigambo, lakini kila hatua yake inaacha alama ya heshima.
Ni kiongozi anayejua nguvu ya upole,
maana kwa wananchi wake nguvu si makelele, bali ni matendo.
Amejenga daraja la imani kati ya
vijana, wazee na wanawake — daraja linalovusha matumaini kuelekea kesho njema.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick
Tluway Sumaye, alipompokea Komandoo huyu wa maendeleo, hakutoa tu mkono wa
pongezi, bali aliona kizazi kipya cha uongozi.
Sumaye alisema kwa tafsiri ya
kimyakimya, “Huyu ni mwana wa maadili, si mwanasiasa wa ahadi.”
Na wananchi walijibu kimya kimya, kwa
heshima na imani: “Ndio, huyu ndiye Lukumay wetu.”
Vita Isiyo na Bunduki
Kwa Arumeru, jina Komando wa Maendeleo halikutolewa kwa bahati mbaya.
Ni heshima aliyoipata kwa kazi yake ya
kugusa maisha, kwa kutenda kimyakimya huku akibadilisha maisha ya watu.
Ameingia kwenye vijiji vyote si kwa magari ya kifahari, bali kwa miguu ya utumishi.
Amezungumza na vijana wa boda boda,
amekumbatia wazee, na kila alikopita ameacha cheche ya matumaini.
Wakati wengine wanasubiri kuapishwa ndipo waanze, Lukumay alianza kabla ya kiapo.
Ametibu, amejenga, amehamasisha,
ameunganisha.
Na sasa, anasimama mbele ya wananchi
wake kama kiongozi tayari, si mgombea anayeomba.
Mkakati wa Kizalendo
Katika moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kampeni, nyumbani kwake, alikutana na viongozi wa kata zote 27 — wenyeviti, makatibu, wenezi na wazee wa kimila.
Alitoa vifaa vya kampeni, lakini
zaidi ya fulana na mabango, aligawa imani.
“Lengo letu si kushinda kwa kura tu, bali kushinda kwa kazi,” alisema kwa sauti ya upole inayotia nguvu.
“Ushindi wa maendeleo, wa barabara,
wa ajira, wa mama wa kitanzania.”
Kauli hiyo ikawasha cheche ya umoja. Wote wakasema kwa sauti moja:
“Komando, tuko nyuma yako hadi mwisho.”
Sauti ya Vijana, Nguvu ya Samia
Dkt. Lukumay amekuwa kiungo muhimu kati ya vijana wa Arumeru na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Ananukuu kwa ujasiri kauli ya Rais
Samia Suluhu Hassan kuhusu fursa za ajira 12,000, akisisitiza kuwa vijana wa Arumeru
hawatabaki nyuma.
Kwa mtazamo wake, maendeleo hayaji kwa makelele bali kwa maombi yenye heshima na juhudi za vitendo.
“Tunaye kiongozi anayeomba kwa
busara, si kwa fujo,” amesema Nicholous Sawa, Katibu Mwenezi wa CCM Arumeru.
Kauli hiyo ikawa ngoma ya matumaini —
vijana wa boda boda, wajasiriamali na wakulima wakasema kwa shauku:
“Komandoo wetu anaongea na Serikali kwa heshima, lakini ana moyo wa chuma!”
Mahaba ya Arumeru
Huko Kiranyi, historia iliandikwa kwa jina moja — Mahaba kwa Mgombea wa CCM.
Wananchi walijitokeza kwa maelfu,
wakiwa wamevaa fulana za “Mama Samia Mitano Tena”, wengine wakiwa na mabango
yenye maandishi makubwa:
“Komando wa Maendeleo Mbele!”
Sauti za wananchi zilisikika kwa hisia, “Tunamchagua Lukumay kwa sababu ametutendea kabla ya kuahidi.”
Haikuwa kampeni ya maneno, bali ya
hisia. Haikuwa siasa, bali ilikuwa shukurani ya wananchi kwa kiongozi wao.
Daktari wa Mioyo na Maendeleo
Kwa wengi, Dkt. Lukumay ni zaidi ya daktari wa binadamu. Ni mganga wa matumaini.
Anasikiliza vilio vya jamii, anapima
mapigo ya moyo ya wananchi wake, na anapendekeza tiba ya kweli — huduma, umoja
na maendeleo.
Wakati siasa nyingine zinajaa mivutano, kwake si vita ya maneno bali ni mbio za matendo.
Kwa chama chake ni mfano wa nidhamu,
kwa wapinzani ni changamoto ya uadilifu, kwa wananchi ni ishara kwamba bado
Tanzania ina viongozi wa kweli.
Siku za Ushindi Zinafika
Leo hii, kutoka Usa River hadi Nkoaranga, kutoka Kiranyi hadi Ngarenanyuki, jina linaloongoza midomo ya wananchi ni moja tu: LUKUMAY!
Wanaimba kwa matumaini, wanaamini kwa mioyo yao yote kwamba
“Komando wetu kashinda, hata kabla ya kura.”
Sasa saa zinahesabiwa, siku zinahesabika.
Si kwa hofu, bali kwa hamasa.
Kwa sababu wananchi wa Arumeru
wameelewa kitu kimoja muhimu —
Maendeleo hayatokani na makelele,
bali na matendo.
Na katika daftari la historia, jina la Dkt. Johannes Lembulung Lukumay litaandikwa kwa herufi kubwa:
Komando wa Maendeleo, mshindi wa vita kabla ya kiapo.
Imeandaliwa na Victor Bariety
0757 856 284



0 Comments