TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SERIKALI YAIPONGEZA TLS KWA KUIBUA HOJA ZA KUPINGA UKATILI KATIKA JAMII.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum Mhe Dkt Doroth Gwajima akiongea katika mdahalo wa kupinga ukatili katika mapenzi na mahusiano uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni wa juma July 23, 2022

Na Urban Epimark, Dar es Salaam.


Serikali imekipongeza Chama cha Wanasheria (Mawakili) wa Tanganyika (TLS) kwa kuwa mstari wa mbele kuibua hoja za kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii na kuzifuatilia utekelezaji wake.


Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawaje na makundi maalum Mhe Dkt Doroth Gwajima mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam wakati aliposhiriki kwenye mdahalo maalum wa kujadili hoja za kupinga ukatili kwenye jamii ukiwemo visa vya mauaji katika mahusiano ya kimapenzia ulioandaliwa wa TLS.


"Chama cha Wanasheria (Mawakili) cha Tanganyika (TLS) ni mfano wa kuigwa  kama walivyo wadau wengine wanao kerwa na tatizo la ukatili wa kijinsia katika jamii na ukubwa wake na hivyo kuibua vuguvugu la hoja za kupinga na kuzisimamia hadi utekelezaji wake" alisema Waziri Dkt Gwajima. 


Dkt Gwajima aliendelea kufafanua zaidi kwamba, endapo kama kuna mtu au kikundi cha watu bado hadi sasa hakijafahamu ukubwa wa tatizo la ukatili wa kijinsia basi ni dhahiri watashindwa kulinda vizazi vya jamii yetu ya kitanzania, aliongeza Waziri.

 

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Prof Edward Hoseah akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa kupinga ukatili kwenye mapenzi na mahusiano ya ndoa uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam July 23, 2022 


Kwa hatua hiyo, Waziri Dkt Gwajima ameiteua na kuiomba TLS kuongoza kamati ya jamii ya ushauri kuhusu kupambana na kutokomeza ukatili wa aina yeyote katika jamii yetu ya kitanzania.


Nae Rais wa TLS Prof Edward Hoseah  kwa niaba ya wanasheria wote,  amepokea pongezi hizo kwa shukrani kutoka serikalini na kuongeza kwa kusema kwamba  kiu yao ni kuwa na Mtaala wa Malezi utakao zingatia elimu ya mapokeo kwa kuzingatia utamaduni wa mtanzania.


"TLS ina mpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa busara zake za kuunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum na kumteua Dkt Doroth Gwajima kuiongoza" alisisitiza Prof Hoseah.

 

Washiriki wa mdahalo wa kupinga ukatili katika mapenzi na mahusiano ulio andaliwa na TLS wakiwa pamoja na wanahabari wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mdahalo huo ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum Dkt Doroth Gwajima, uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam July 23, 2022 


Prof Hoseah alimwomba Waziri Dkt Gwajima kusaidia kupatikana kwa mtaala wa elimu utakaozingatia zaidi malezi ya vijana na watoto ili wafunzwe na kuelewa malezi ya kuheshimu haki za jamii ikiwemo jinsia na mahusiano zitazo zingatia utamaduni wa kitanzania.


Kwa upande wa madhehebu ya dini, Mchungaji mstaafu wa KKKT Richard Hananja alisema, tatizo lililopo ndani ya Jamii ni ukombozi wa kifikra ambazo zimesababisha Jamii kuingia katika janga kubwa na zito la vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa wito kwa jamii iamke na kujikomboa kifikra.

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum Mhe Dkt Doroth Gwajima (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mdahalo wa kupinga ukatili katika mapenzi na mahusiano. Wengine ni Rais wa TLS Prof Edward Hoseah (kushoto) na Mkurugenzi wa kituo cha Haki za Binadam nchini Bi Anna Henga (kulia) baada ya kumalizika mdahalo huo July 23, 2022 


Nae Mkurugenzi wa kituo cha Haki za Binadam hapa nchini Anna Henga alisema, kwa sasa hali ya ukatili imekithiri kwani kati ya wanandoa 10, sita kati yao wanapitia ukatili hivyo akaiomba jamii kubadili mtizamo kwani unyanyasaji wa kijinsia hauna nafasi yeyote kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments