TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BINGWA WA JUMUIYA YA WAZAZI ATIMIZA AHADI YAKE YA KUTOA KADI ZA CCM ZA JUMUIYA YA WAZAZI SENGEREMA

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Sengerema Jackson Mazinzi akizungumza na wananchama wa jumuiya hiyo muda mchache alipochaguliwa katika mkutano mkuu wa ccm na kutoa kadi za ccm elfu mmoja alizozihaidi wakati akiomba kura 

Anna Ruhasha, Mwanza.

Mweyekiti wa jumuiya ya wazazi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilayani Sengerema mkoani Mwanza  Jacksoni Mazinzi  ametoa kadi  za   CCM Elfu Moja  za jumuiya ya wazazi   kwaajili ya  kupunguza changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa kadi kwa wanachama wa jumuiya hiyo.

Mazinzi ametoa kadi hizo wakati akitekeleza ahaadi yake mbele ya wananchama wa jumuiya hiyo aliyoiahidi wakati akiomba kura ya  za ndiyo katika uchaguzi mkuu ndani ya ccm ya  kutafuta viongozi katika jumuiya hiyo.

Aidha katika uchaguzi huo ulifanyika   mwishoni mwa wiki iliyopita  na kufanyikia katika ukumbi wa Sengerema sekondari Mazinzi alitangazwa kuwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi  Mwashamu Ismail kuwa Mazinzi alipata kura 371

Hata hivyo Mazinzi akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua  amesema kuwa katika uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano atahakikisha anapunguza changamoto zinazozikabili jumuiya hiyo .

“nimeamua kugombea nafasi hii kwa sababu nimebaini jumuiya hii imekuwa  ikikabiliwa na  changamoto kama vile uelewa juu ya mambo Kadha wa kadha ya jumuiya  niwaambie wanancha nitaanza kutoa semina kwenu “Mazinzi.

Ali kadhalika aliyekuwa mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charlse Tizeba  mmoja ya wachaguliwa  katika uchaguzi huo  ambapo amechaguliwa kuwa mwakilishi mkutano mkuu taifa kupitia jumuiya ya wazazi  pia  akizungumza na wapiga kura baada ya kutangazwa kuwa mshindi amesema  ataitumikia jumuiya hiyo kwa ufasaa kutokana na uzoefu alionao hasa katika kudumisha umoja  kwa wanancha.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Sengerema mkoani humo  Agustine Makoye amesema kuwa uchaguzi  ulifanyika ni kwamujibu wa katiba ya chama ,uku Katibu wa chama hicho wilaya Muksin Zikatimu ameongeza kuwa uchaguzi ngazi za jumuiya umeisha na kuwata viongozi waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za chama kwa weledi.

 Mwisho

Post a Comment

0 Comments