![]() |
| Consolatha Charles Malunde mshindi wa kwanza Baraza wilaya kwa kuibuka na kura 365 kati ya kura zilizopigwa 552. |
ANNA RUHASHA-MWANZA
Viongozi wa jumuiya ya wananwake wa chama cha Mapinduzi CCM wilayani Sengerema mkaoni mwanza Wamesema kuwa watahakikisha wanasimamia yale yote waliyoahidi kuyatekeleza katika uongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano.
Hayo yamezungumzwa na baadhi ya viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu ndani ya chama cha mapinduzi CCM katika jumuiya ya wanawake wilayani Sengerema mkaoni humo.
Akizungumzia kwa niaba ya wenzake mmoja ya wagombea ambae ameibuka mshindi nafasi ya mjumbe Halmashauri kuu wilaya Consolatha Malunde.
Amewashukuru wajumbe kwa kumuamini kumpa nafasi hiyo licha ya kutumikia nafasi mbali mbali katika chama hicho “nawashukuru kwa kupigiwa kura zaidi 346 na kuwa mshindi wa kwanza kati ya wagombea 21 ambao tuliwania nafasi hii wajumbe hawa nitawalipa kwa kufanya kazi kwa weledi " amesema Malunde.
Aidha ameongeza kuwa jumuiya ya wanawake ni jumuiya yenye miradi mingi ya maendeleo kwa kushirikiana na viongozi waliochaguliwa atatoa ushirikiano ili kuhakikisha jumuiya inapiga hatua zaidi.
Katibu wa UWT wilaya Rosemary Mwakasalo amesema kuwa uchaguzi umefanyika kwa amani na kumalizika salama ambapo amesema kuwa jumuiya ya wanawake imechagua kiongozi ngazi ya wilaya ,mjumbe wawakilishi ngazi ya wilaya na mkoa , wajumbe wa halmashauri kuu wilaya pamoja na mwakilishi ngazi ya Taifa.
Mwisho

0 Comments