TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

HALIMA HASSAN M/K MPYA WAZAZI WILAYA YA MBOGWE.

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita Bi Halima Hassan (pichani), amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu kwa kupata kura 180 dhidi ya kura 310 zilizopigwa na kumshinda mpizani wake wa karibu aliyepata kura 100 huku kura 19 zikiharibika katika uchaguzi uliofanyika jana Sept 25, 2022.

Na Urban Epimark, GEITA.

Mwanachama wa CCM Halima Hassan (39) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Wazazi katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na kuwashinda wenzake watatu katika uchaguzi uliofanyika  wilayani Mbogwe jana Sept 25, 2022

Halima Hassan ambae kwa umri wake bado ni mwanamama nae kuwa na mchanga zaidi kuwashinda wagombea wenzake alijizolea kura 180 dhidi ya kura 310 za wajumbe wote waliopiga kura huku akifuatiwa na mpizani wake wa karibu aliyepata kura 100 huku kura 19 zikiharibika.

Akitangaza matokeo hayo jana jioni kwenye ukumbi wa uchaguzi huo wilayani Mbogwe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mhe Yusuf Mohamed aliwapongeza wajumbe wa mkutano huo kwa jinsi walivyotumia fursa na demokrasia ndani ya chama kuchagua viongozi wao.


Mwenyekiti mstaafu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Mbogwe Bw Isaya Chapakazi (pichani) akiongea kwenye mkutano huo wa uchaguzi kabla ya wajumbe hawajapiga kura kuchagua viongozi wengine jana Sept 25, 2022

Pia aliwapongeza wajumbe kwa kuchagua mwanamama ambae alisema wamefuata nyayo za Mwenyekiti wao wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwataka wale wengine ambao kura hazikutosha wasikate tamaa bali waendelee kutoa ushirikiano ili kipindi kingine wagombee tena.

Halikadhalika Msimamizi huyo wa uchaguzi alimpongeza Mwenyekiti anaeondoka (Mstaafu) Bw  Isaya Chapakazi kwa uongozi mzuri na pia kwa kuweza kuandaa viongozi watakao ongoza jumuiya hiyo baadae yake na kusema wagombea wote walikuwa wazuri.


Wagombea wanne wa uchuguzi huo wa jumuiya ya wazazi (CCM) katika nafasi ya Mwenyekiti wakiwa wamesimama mbele ya wajumbe wakiwa wameshikilia shahada zao kabla ya uchuguzi huo kufanyika jana Sept 25, 2022

"Hongera sana Mwenyekiti wangu mstaafu. Nitakumiss Sana ofisini. Kwa kipindi kifupi nilichokuwa na wewe umenilea vizuri mno. Lakini tayari umenikabidhi Kwa mwenyekiti mpya hakuna jinsi ndio utaratibu uliowekwa na chama. Naamini Jumuiya umeiacha salama kwenye mikono ya Mwenyekiti mahili na Mama Shupavu Ndg Halima Hsaan Chembamoyo" 

"Niwapongeze Sana wajumbe wa mkutano mkuu wa wazazi Wilaya ya Mbogwe kwa umakini wenu mkubwa kwani ilikuwa kazi ngumu. Jumuiya yetu ilipata wagombea wazuri  mno, na wenye uwezo mkubwa na sifa za kuwa kiongozi, hata mimi kwenye kura yangu ilinipa ugumu kuamua vema yangu niiweke kwa nani, nilitamani kuwawekea wote wanne lakini nikaogopa kuharibu kura yangu. Lakini wote walikuwa wanafaa hivyo uchaguzi umekwisha, tumeshapata viongozi wa Jumuiya yetu sasa tuwape ushirikiano" alisema Msimamizi wa uchaguzi.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuiya ya wazazi (CCM) wilaya ya Mbogwe katika mkoa wa Geita wakiwa tayari ukumbini wakimsikiliza Msimamizi wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mhe Yusuf Mohamed (hayupo pichani) hapo jana Sept 25, 2022.

Nae huyo Mwenyekiti mpya wa wazazi wilaya ya Mbogwe Bi Halima Hassan aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wao na kusema atarudisha imani waliompatia kwa kuwatumikia vizuri.

Viongozi wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na 

Bw John Ntungwa Mbonea kwa nafasi ya Katibu wa wazazi wilaya, mwingine ni Wilson  Lutalicha Mpuya ambae ni Katibu wa Elimu na Mazingira na  kwa nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri ya CCM wilaya ilienda kwa Bi Odilia  Maholelo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments