TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MKUU WA WILAYA GEITA AHIMIZA CHANJO KUWAFIKIA JAMII YA WAFUGAJI NA WACHIMBAJI MADINI GEITA.

Mkuu  wa wilaya Geita Wilson Shimo akiwahimiza wazazi na walezi kujitokeza kwa wing kuwaleta watoto wao iliwaweze kupatiwa chanjo ya Polio zoezi lililoanza leo Septemba 1 hadi 4, 2022.

Na Editha Edward, Geita.

MKUU wa wilaya Geita Wilson Shimo amewataka  wahusika na zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 iliyoanza September 1 hadi September 4, 2022  kuhakikisha wanayafikia maeneo yote ambayo yameainishwa na kutambuliwa na wilaya hiyo yakiwemo maeneo ya wafugaji na wachimbaji.

Shimo alisema hayo alipo kuwa akifungua  kikao cha afya ya msingi ya jamii juu  ya kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu ilikufikia lengo la utoaji wa chanjo ya polio kuwafikia watoto chini ya miaka 5 katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa katika kampeni hiyo licha yakuwafikia  watoto wa maeneo mengine wanakwenda kuweka mkazo kwa wafugaji na wachimbaji ambao wanahamahama pamoja  nakuingia wapya katika maeneo hayo ili watoto wao wawezekupatiwa chanjo ya polio awamu ya tatu.

Mkuu huyo wawilaya aliwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuwaleta watoto wao iliwaweze kupatiwa chanjo hiyo kwani chanjo hiyo haina madhara yoyote bali ni chanjo salama ambayo inawalinda watoto iliwasiweze kupatwa na ugojwa huo wa Polio.

Kwaupande wake mratibu wa Chanjo wilaya ya Geita Jalio Munyi alisema kuwa chanjo hiyo itatolewa ndani ya siku nne na wanatarajia kuchanja watoto  250,487 katika halmashauri ya Wilaya ya Geita  huku wakitarajia kuchanja watoto 78774 katika halmashauri ya Mji Geita.

Aliwataka wananchi wawilaya ya Geita kujitokeza ili zoezi hilo liweze kwenda vyema kwani tayari wataalamu wa kutoa chanjo hizo wapo wakutosha na  watoto wote chini ya umri huo watapatiwa chanjo kwa wakati.

“Tuwalinde watoto wetu mapema kwa chanjo ya polio kwani ugojwa huo umekuwa tishio kwa miaka mingi hivyo tuepukane na imani potofu kuwa chanjo hiyo inamadhara jambo ambalo silakweli chanjo hiyo nisalama na haina madhara yoyote" alisema mratibu huyo.

Fredrick Masalu nimwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela alisemakuwa wao kama wenyeviti watawahamasisha wananchi na kuhakikisha zoezi hilo linaenda vizuri na kuwapa elimu wananchi kuwa chanjo hizo hazina madhara nisalama iliwatoto wao waweze kupata kinga ya ugojwa huo wapolio.

MWISHO;


Post a Comment

0 Comments