TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU


Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga  akizungumza na katika mkutano wa pili wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari binafsi na  serikali.

Na Anna Ruhasha, Mwanza

 Mkuu wa Wilaya  ya Sengerema  mkoani Mwanza  Senyi Ngaga    amesema kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto katika sekta ya Elimu  kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.

Dc ametoa kauli hiyo wakati akizungumza  katika mkutano mkuu wa umoja wa wakuu wa shule za Sekondari na binafsi  mkao wa mwanza alipokalibishwa kama mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa wakuu wa shule mkoa wa mwanza TAHOSA akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa wiliya ya Sengerema.

Aidha amesema kuwa serikali bado inatoa  fedha katika kuboresha miundombinu ya elimu ambapo ameongeza kuwa  serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa  na walimu katika kusimamia  elimu na kuhakikisha ufahuru  unaongezeka mwaka hadi mwaka.

Kuna changamoto mmezibainisha hususani kwa  shule za serikali ,uhaba wa mabweni na Walimu wa Sayansi nk’lakini nyinyi ni Mashahidi mmeona serikali ya Mama Samia fedha za Uviko  ujenzi wa vyumba vya Madarasa   , ajira  zimetolewa nyingi za walimu  lakini  niseme serikali haijalala bado changamoto hizo mlizozisema serikali inaendelea kushugulika nazo.”amesema Dc Ngaga.

Wakuu wa shule walioshiriki katika mkutano huo uliofanyika katika chuo cha maendeleo ya wananchi FDC mjini Sengerema mkoani Mwanza.

Hata hivyo mwenyekiti wa umoja wa wa wakuu wa shule za sekondari binafsi na  serikali Deus lugwala  amesema kuwa mbali na changamoto za uhaba wa miundombinu za kujifunzia na kufundishia kwa baadhi ya shule   wamesema kuwa umoja huo ulianzishwa kwa lengo la  kujengeana uwelewa  na kusimamia nidhamu kwa wakuu wa shule hao.

Wakuu wa shule walioshiriki katika mkutano huo uliofanyika katika chuo cha maendeleo ya wananchi FDC mjini Sengerema mkoani Mwanza.

Baadhi ya wakuu wa shule wananchama mkuu wa shule ya sekondari kilabela leornad Manyoni akizunguma kwa niaba ya wenzao amesema kuwa umoja huo umewajenga kiutendaji na kinidhamu katika kusimamia taluma na maadili  katika kazi.

Hata hivyo mkutano mkuu wa pili umeenda sambamba na uchaguzi wa kuwachagua viongozi  watakao ongoza kwa miaka mitano ijayo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments