TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SERIKALI YAKEMEA TABIA YA UTOROSHAJI MADINI.

Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko akitoa hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita leo October 03, 2022. Kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini mikoa wa Geita (GEREMA) Bw Christopher Kadeo.

Na Urban Epimark, GEITA.

Serikali imesema haita mvumilia yeyote anae jihusisha na utoroshaji wa madini hapa nchini na pia wale wasiofuata utaratibu na sheria zilizowekwa za kusimamia uuzaji wa madini katika masoko rasmi na kuwataka waache tabia hiyo mara moja.

Ameyasema hayo leo mjini Geita Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko wakati alipokuwa Mgeni Rasmi akimwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji. 

"Hapa nchini pameanza kuibuka wimbi la baadhi ya wafanyabiashara wa madini kutorosha baadhi ya madini kwenda kuyauza kwingine bila kufuata mfumo rasmi wa masoko ya kuuzia madini. Natoa wito kwao waache mara moja kwani wanahujumu harakati za serikali kuboresha sekta ya madini" alisema Waziri Dkt Biteko.

Baadhi ya washiriki walio hudhuria hafla ya uzinduzi wa maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita wakimsikiliza Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo October 023, 2022

Mhe Dkt aliendelea kueleza zaidi kwamba, hakuna sababu yeyote ya wao kufanya hivyo kwani tayari serikali ilisha fanyia kazi changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya madini ikiwemo ukosefu wa masoko rasmi, bei ya kuuzia, mfumo wa kulipa kodi.

Halikadhalika Waziri Dkt Biteko alitaadharisha wale wanao tumia njia zisizo sahihi na zisizo za kiteknolijia kwa kufifisha ubora wa dhahabu wakati wa uchenjuaji kwa kutumia teknolojia dhaifu au duni mfano ubora wa Dhahabu ambayo ungetakiwa uwe asilimia 93 ya ualisia (purity) wao kwa kutumia njia zingine wana sababisha kupata ubora wa chini wa asilimia 83 na kusababisha upotevu wa thamani.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela alipokuwa akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita leo October 03, 2022

Waziri amewataka wenye tabia hizo serikali itawafuatilia na kuendelea kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafilisi pamoja na vifungo gerezani.

Nae Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela amewaonya watumishi wa serikali wenye dhamana ya kuwashughulikia wale wanao kuja kuomba kupatiwa maeneo ya kuwekeza kwenye madini waache kuwazungusha na kuwakatisha tamaa wanapo tafuta vibali.

Wadau mbalimbali wa shughuli za madini walio hudhuria hafla ya uzinduzi wa maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko (hayupo pichani) mjini Geita leo October 03, 2022

Mhe Shigela ametoa kauli hiyo wakati akitoa hotuba yake ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Madini Mhe  Dkt Doto Biteko ili azindue maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji leo mjini Geita.

Awali, Mgeni Rasmi ambae alimwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye ndie alipaswa kuwa Mgeni Rasmi lakini akatingwa na kazi nyingine, Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko alitembelea maonesho hayo na kujionea jinsi wadau mbalimbali katika sekta ya madini wanavyo tumia sayansi na teknolojia katika shughuli za uchimbaji madini na kuwapongeza.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi Zahara Michunzi (mwenye kilemba cha rangi ya zambarao) akiwa ameketi kwenye jukwaa kuu na wageni wengine akimfuatilia Mgeni Rasmi Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko wakati akitoa maagizo kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Mji pamoja na Mbunge kubuni namna ya kuweka vichocheo (incentives) kwa wanaokuja kuomba kuwekeza katika sekta ya madini, wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho leo October 03, 2022

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini  mkoa wa Geita (GEREMA) Bw Christopher Kadeo alimweleza Waziri wa Madini kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wameanza kujihusisha na utoroshaji wa madini bila kufuata mfumo rasmi wa soko ulio wekwa na serikali. 

Aina ya mitambo ya kisasa ya uchimbaji madini inayo milikiwa na kampuni ya uwekezaji ya GGML ya mjini Geita ikiwa kwenye maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji leo October 03, 2022

Wataalam wa kazi za utafutaji na uchimbaji madini wakiwa kwenye moja ya mabanda ya makampuni mbalimbali yanayo jishughulisha na kazi za madini yaliyo shiriki kwenye maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita leo October 03, 2022


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments