TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

STAMICO KUBEBA AGENDA YA KUTUNZA MAZINGIRA NCHINI.

Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais anaye shughulikia Mazingira Dkt Suleiman Jafo akitoa maagizo kwa STAMICO kuzalisha mkaa mbadala wa kutosha ili Wakala wa Misitu nchini (TFS) wapunguze kutoa vibali vya kukata mita kwa uchomaji mikaa. Pembeni yake anae pokea maagizo hayo ni Meneja wa Masoko & Mawasiliano wa STAMICO Bw Godfrey Meena leo October 06, 2022

Na Urban Epimark, GEITA.

Shirika la Madini Nchini (STAMICO) limesema litaibeba agenda ya kutunza mazingira nchini kwa kutengeneza mkaa mbadala kwa wingi ili kuzuia ukataji wa miti unaofanyika nchini ili kupata nishati ya kupikia aina ya mkaa wa kawaida.

Pia STAMICO imesema inakusudia kujenga viwanda viwili vikubwa vya kutengeneza mkaa mbadala eneo la Kibaha mkoani Pwani na Kiwira kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kuzalisha mkaa huo vyenye uwezo wa kuzalisha tani elfu 20 kwa saa kila kimoja.

Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa STAMICO Bw Godfrey Meena alimweleza Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira Dkt Suleiman Jafo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mkoani Geita.

Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira Dkt Suleiman Jafo (kulia) akimshuhudia Meneja wa Masoko & Mawasiliano wa STAMICO Bw Godfrey Meena (kushoto) pamoja na Afisa Usalama wa STAMIGOLD kutoka Mgodi unao milikiwa na STAMICO wa Biharamulo Bw Fred Makwebeta (kulia) kupanda mti katika eneo la viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita leo October 06, 2022

"Mbali na STAMICO kuwa na jukumu la kuwalea wachimbaji wadogo ili wakue wawe wa ngazi ya kati hadi wakubwa, tunalo pia jukumu la kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yanapofanyika machimbo ya madini lakini pia kwa kutumia utaalam mwingine wa kutengeneza mashimo ya kuingilia migodini badala ya kutumia miti" alisema Meneja Masoko Bw Meena.

Nae Afisa Mwandamizi anae shughulikia Usalama maeneo ya migodi katika mgodi unao milikiwa na STAMICO wilayani Biharamulo mkoani Kagera wa STAMIGOLD Bw Fred Makwebeta amemkaribisha Waziri wa Mazingira Mhe Dkt  Suleiman Jafo kutembelea mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo ili kujionea jinsi STAMIGOLD inavyo tunza mazingira na kuokoa ukataji miti.

Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira Dkt Suleiman Jafo (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Wilson Shimo (pembeni yake kulia) akipatiwa maelezo kuhusu shughuli za STAMICO kutoka kwa Mhandisi Tiberio Kaduma wakati Waziri Dkt Jafo alipotembelea banda la STAMICO leo October 06, 2022. Wa kwanza kulia (walio simama mwenye kofia) ni Meneja Masoko & Mawasiliano wa STAMICO Bw Godfrey Meena.

Waziri Dkt Jafo amepongeza juhudi kubwa na nzuri zinazofanywa na STAMICO katika agenda ya kutunza mazingira hapa nchini na kuwataka STAMIGOLD kutengeneza mkaa mbadala wa kutosha kukidhi mahitaji ya nishati mbadala nchini.

Halikadhali Dkt Jafo  amewataka STAMIGOLD kuvitumia vikundi vya akina mama kwa kuwawezesha kufunga mitambo kila Halmashauri ili watengeneze mkaa mbadala wa kutosha na kufanya wakala wa misitu nchini (TFS) kupunguza utoaji vibali vya kukata miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa jambo ambalo amesema linachangia uharibifu wa mazingira ulio mkubwa.

Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira (kulia mwenye tai) akipatiwa maelezo na Meneja Masoko & Mawasiliano wa STAMICO Bw Godfrey Meena (aliyeshika kipaaza sauti) kuhusu ubora wa mkaa mbadala unao tengenezwa na STAMICO wakati Waziri Dkt Jafo alipo tembelea banda la STAMICO kwenye maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji yanayoendelea mji Geita leo October 06, 2022

Awali Meneja wa Masoko na Mawasiliano  wa STAMICO Bw Godfrey Meena alimweleza Waziri wa Mazingira Mhe Dkt Suleiman Jafo kwamba STAMICO imepanga kupanda miti Elfu 10 kwa kuanzia mkoa wa Dodoma hadi kuja mpaka mkoani Geita.

Kwa sasa STAMICO ipo kwenye kampeni ya kuutangaza mkaa mbadala inao utengeneza kutoka STAMIGOLD unaoitwa "Rafiki Briquettes" ambao una nguvu mara tatu ya mkaa wa kawaida na unauzwa kilo moja kwa shilingi elfu moja katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji yanayo endelea mjini Geita.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments