TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO NSSF

Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira Mhe Dkt Suleiman Jafo (kushoto) akiongea na Meneja wa NSSF mkoa wa Geita Bi Winiel Lusingu (kushoto) wakati alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji mjini Geita leo October 06, 2022

Na Urban Epimark, GEITA.

Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais anae shughulikia Mazingira Dkt Suleiman Jafo leo October 06, 2022 ametembelea banda NSSF katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini na uwekezaji na kuitaka NSSF kuleta ofisini kwake mpango kazi wa jinsi watakavyo muunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la kutunza mazingira.

Halikadhalika Dkt Jafo amewataka NSSF katika mpango kazi wao huo, waeleze watasaidiaje  upatikanaji wa vizolea taka (Dust bins) na kwa idadi gani ambavyo vitatumiwa na Halmashauri zetu hapa nchini kubadilisha tabia kwa jamii katika kampeni ya kutunza mazingira ili mtu akila ndizi, ganda atupe kwenye Dust bin na si kutupa kila mahali na kuchafua mazingira.

Awali akimkaribisha Waziri Dkt Jafo, Meneja wa NSSF wa Mkoa wa Geita Bi Winiel Lusingu amemweleza Waziri wa Mazingira kwamba, kwa sasa NSSF inashirikiana na taasisi zingine za SIDO, Azania Bank, VETA na NEEC katika kutekeleza program ya kukopesha sekta binafsi wakiwemo wachimbaji wadogo katika kutunza mazingira ijulikanayo kama "SANVN"

Katika program hiyo NSSF inatoa mikopo kwa wachimbaji wadogo wadogo kupata mitaji ya uchimbaji na pia kutunza mazingira. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments