TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WAZIRI KUTOKA ZAMBIA AZURU GEITA


Muwakilishi wa Waziri Wizara ya Maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati kutoka Zambia Kennedy Mumba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na uwezeshaji akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Chama Cha wachimbaji madini wanawake Mkoa wa Geita (GEWOMA), kulia alivaa kofia ngumu ni Asia Hussein Mwenyekiti wa GEWOMA alipotembelea kwenye maonesho ya 5 ya kitaifa ya Teknolojia ya Uwekezaji kwenye sekta ya Madini mjini Geita leo 1 Oktoba 2022.

Na Beatus Bihigi, Geita.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Uwezeshaji kutoka Wizara ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Vya Kati kutoka Nchini Zambia ametembelea Mabanda ya Maonyesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini.

Muwakilishi wa Waziri kutoka Zambia Kennedy Mumba (Shati la drafts) akipata maelezo fasaha juu ya shughuli za GGML kutoka kwa Meneja mawasiliano na mahusiano ya umma wa Mgodi huo Stephen Mhando (alieshika kipaza sauti) leo 1 Oktoba,2022

Mkurugenzi huyo ametembelea Mabanda yenye Vifaa vya Kisasa Kutoka Mgodi wa Geita(GGML) na migodi ya wachimbaji wa kati na wadogo na kushuhudia Vifaa hivyo vinavyofanya kazi kwenye maeneo ya migodi wakati wa uzalishaji wa madini ya dhahabu.

Muwakilishi wa Waziri kutoka Zambia Kennedy Mumba alievaa  Shati la drafts akipata maelezo na Geofrey Meena ambaye ni Meneja Masoko na mahusiano ya umma katika banda la STAMICO leo 1 Oktoba 2022.

Aidha,ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo kwa kuonyesha shughuli wanazofanya kupitia maonesho hayo,ambapo ameahidi kwa mara nyingine Zambia kushiriki maonyesho hayo.

Pichani ni Ruth Eric Muguras Mhandisi wa miamba na vilipuzi (Drill &Blast Engineer) kutoka GGML akifafanua tabia za miamba ya Dhahabu kwa mgeni rasmi raia wa Zambia alipotembelea banda hilo akimuwakilisha Waziri wa viwanda na biashara wa Zambia (hayupo Pichani)

Muwakilishi wa Waziri wa viwanda biashara na Uwekezaji kutoka Zambia amepata wasaa wa kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ikiwemo banda la GGML,banda la benki kuu ya Tanzania (BoT), STAMICO , GEREMA , GEWOMA, Blue Coast na banda la kliniki ya Biashara ambapo amekiri kujifunza mengi mazuri ambayo atayafikisha kwa wafanya biashara wa Zambia. 

Mwakilishi wa kampuni ya usafishaji akielezea ambayo kampuni hiyo ya Blue Coast inavyo toa huduma kitaifa na kimataifa mbele ya Kennedy Mumba kutoka Zambia.

Banda la GGML mmoja wa Maofisa wake akielezea upatikanaji wa madini ya Dhahabu kitaalam zaidi mbele ya Kennedy Mumba muwakilishi wa Waziri wa Maendeleo ya viwanda na biashara wa Zambia.


Kennedy Mumba alievaa Shati la drafts katikati akiwa katika picha ya pamoja, kulia kwake ni Mwenyekiti wa GEWOMA Bi Asia Hussein,Afisa biashara halmashauri ya Mji Geita na Afisa wa bank Kuu ya Tanzania na kushoto kwake ni maafisa aliambatana nao kwenye maonesho ya madini Geita leo 1 Oktoba 2022.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments