TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

SISTA HEDWIGISI MGONDO;MTAWA ANAE LISHUKURU KANISA KWA MALEZI.

Sr Hedwigisi Mgondo, ana mshukuru Mungu kwa zawadi ya Utume na pia kanisa kwa malezi mazuri.

Na Urban Epimark, GEITA

Sista Hedwigisi Mgondo ni mwenyeji wa kutoka parokia ya Kowak, Jimbo Katoliki la Musoma na alizaliwa mwaka 1975 na mwaka 2022 alitimiza miaka 25 ya Utawa tangu aweke nadhiri za daima za kumtumikia Mungu kupitia utume wa kanisa kama mtawa wa kike.

Sr Hedwigisi Mgondo ambae anafanya utume wake katika Jimbo Katoliki la Geita, katika parokia ya Bikira Maria wa Fatima, January 29, 2023 ana mshukuru Mungu pamoja na wakristo wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima ambapo tangu mwaka 2012 ndipo alipo ripoti rasmi jimboni humo.

"Nina lishukuru kanisa pamoja na uongozi wake wote, akiwemo Baba Askofu Flavian Kassala, Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita pamoja na maparoko wote waliopita parokia ya Bikira Maria wa Fatima lakini kwa sasa akihudumu Paroko, Padre Gerald Singu, nina washukuru sana.

Halikadhalika nawashukuru masista wenzangu katika shirika la masista wa Bibi yetu wa Kilimanjaro (CDNK) pamoja na wazazi wangu kwa kunilea kwa malezi mazuri, hadi leo nipo kama nilivyo" alisema Sista Hedwigisi Mgondo. 

Sr Hedwigisi Mgondo (kulia) akiwa na viongozi katika Halmashauri ya Walei, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita anako fanya Utume wake. Kutoka kushoto ni Mr Sebastian Cosmas, Mwenyekiti wa mtaa wa Msufini akifuatiwa na Mr George Kalenda, Mwenyekiti wa mtaa wa Msalala Road, wote kutoka Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Geita.

Akiwa katika Jimbo Katoliki la Geita, ambapo hadi sasa (mwaka 2023) anatimiza miaka 10 ya utumishi  jimboni humo baada ya kufanya kazi katika Jimbo Katoliki la Moshi na baadae Jimbo la Arusha kisha kuhamishiwa Jimbo Katoliki la Geita,  kitaaluma ni mwalimu wa masomo ya ufundi (VTC)  upande wa ufumaji nguo.

Akiwa parokiani Jimbo la Geita, parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Sista Hedwigisi Mgondo amekuwa akifanya malezi yake kama Sista mlezi katika mitaa miwili ya Msufini na Msalala Road. 

"Ninawashukuru kwa namna ya pekee wana mitaa hii miwili ya Msufini na Msalala Road kwa jinsi mlivyo nipokea na kunisaidia katika utume wangu kama mlezi wenu. Mbali na kuniombea katika sala zenu, pia mliniimarisha katika utume wangu, Mungu awabariki sana" alisema Sr Hedwigisi Mgondo. 

Aliendelea kueleza kwa furaha kwamba, wakati alipofika, mitaa hii miwili (ya Msufini na Msalala Road) haikuwa katika mwamko mkubwa wa mambo ya kanisa lakini kwa sasa anapo sherekea Jubilee yake ya miaka 25, ambapo wakristo wa mitaa hiyo ndio walio mwandalia sherehe hiyo ya Jubilee,  anasema ameona Mungu alivyo wajalia mwamko mkubwa wa kiimani katika kumtumikia Mungu kupitia kanisa.

Ameendelea kufafanua kwamba, katika malezi yake katika parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita miito mitakatifu ikiwemo wito wa ndoa, wito wa utawa wa kike na kiume, Mungu aliichepusha na hadi sasa ndoa nyingi zimefungwa na vijana baadhi wa kike na kiume wapo katika malezi, kusomea miito mitakatifu katika mashirika mbalimbali ya kitawa.

Mbali na mafanikio hayo, anasema Sista Hedwigisi Mgondo kwamba, zipo pia changamoto alizokutana  nazo wakati wa malezi katika mitaa ya Msufini na Msalala Road mjini Geita. 

Kitaaluma Sr Hedwigisi Mgondo ni mwalimu wa ufundi katika moja ya vyuo vya ufundi (VTC) vinavyo endeshwa na Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Katika picha, Sr Hedwigisi Mgondo yupo kwenye moja ya kiwanda cha ufumaji nguo (masweta ya wanafunzi) ambapo yeye ni mwalimu na pia ni fundi mtaalam wa mashine hizo.

Moja ya changamoto kubwa ni wenyeji wanaoishi mitaa hiyo kubadilisha maeneo ya kuishi kila baada ya muda mfupi kwa kuhamia maeneo mengine. Hii inafanya mikakati inayo pangwa na kanisa kwenye mitaa hiyo kutotimia kwa wakati ulio pangwa.

Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Msalala Road, Bw George Kalenda kwa niaba ya mitaa yote miwili ya Msufini na Msalala Road ametoa shukrani nyingi kwa Mungu kwa zawadi ya utume wa Sista Hedwigisi Mgondo kwani katika malezi yake, ameongeza hamasa na chachu zaidi kwa wana mitaa hiyo kulipenda kanisa na kulitumikia.

Bw George Kalenda alimalizia kwa kumtakia Sista Hedwigisi Mgondo utume mwema kadiri ya Mungu atakavyo mjalia uhai hapa duniani.

Sr Hedwigisi Mgondo akiunganisha nyuzi kwenye mtambo wa kufuma nguo (masweta ya wanafunzi) uliopo mjini Geita. Sr Hedwigisi Mgondo anasherekea Jubilee ya miaka 25 ya Utume wake na wana parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita, January 29, 2023.

Sista Hedwigisi Mgondo anatarajiwa kufanyiwa sherehe ya Jubikee ya miaka 25 ya kumpongeza parokiani hapo January 29, 2023 siku ya Dominika ya 4 ya mwaka wa kanisa ambapo Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhashamu Flavian Kassala pia anategemewa kushiriki.

Sista Hedwigisi Mgondo ana mshukuru Mungu kwa zawadi ya Utume alio ufanya kwa mitaa ya Msufini na Msalala Road, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Jimbo Katoliki la Geita na kusema "Ahsante Mungu kwa vile wewe ndio uliye niwezesha niwe kama nilivyo kwa Jubilee ya miaka 25 ya Utawa"


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments