TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

KATIBU MKUU CCM, DKT. NCHIMBI AAGIZA OFISI YA MKUU WA MKOA GEITA KUSHUGHULIKIA KERO ZA WANANCHI.

 

Na: Samwel Masunzu Geita

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM  Taifa balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita kuhakikisha inashughulikia kero ambazo zimepokelewa kutoka kwa wananchi wa mkoa huo

Dkt. Nchimbi akiwa katika halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita kwenye  mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Uwanja kata ya Nyankumbu, amesema wamepokea na kusikiliza kero 48 kutoka kwa wanachi 34

Amesema wataendelea kufuatili kwa kila mmoja aliyewasilisha kero yake ili kujua kama kero aliyoiwaslisha imeshughulikiwa ipasavyo

“Moja ya mambo tunayoyafanya ni kusikiliza kero za wananchi kwa maeneo yote tulipopita, na lengo ni kusikiliza yale ambayo wananchi wanayo na wanatamani yafanyiwe kazi, na nitumie nafasi hii kukukabidhi kero hizi  Mh. mkuu wa mkoa na uhakikishe kero zote zinapatiwa majibu”. Alisema Dkt. Nchimbi




Balozi Dkt. Nchimbi (Katibu Mkuu CCM-Taifa) akiwa na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM. 

Alisema,  serikali itaendelea kuhakikisha inaboresha huduma bora kwa wananchi kwa kutenga bajeti katika sekta zote zikiwemo elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na umeme

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akipokea  kero hizo alieleza kuwa, katika mkutano wa agosti 12 mwaka huu 2024 uliofanyika kwenye mamlaka ya mji mdogo wa Katoro  halmashauri ya wilaya ya Geita, zaidi ya kero 160 zimepokelewa kwenye mamlaka hiyo, na kero nyingine zimepokelewa katika halimashauri ya wailaya ya Chato.

Shigela alieleza kuwa, kero hizo atahakikisha zinataftiwa ufumbuzi na kuwaslisha majibu yote kwa wanananchi  hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa agosti

“Kwanza kabisa nikushukuru wewe Katibu mkuu kwa kutumia mfumo wa kisayansi kupata kero kutoka kwa wananchi, lakini pia nimshukuru Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kunipatia wasaidizi wenye weledi ambao ni ma DC, ma DAS na wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote chini cha RAS na kiukweli wanatekeleza wajibu wao vizui sana, jambo la pili nikiri kupokea kero hizi na nitazifanyia kazi hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa agosti.” Alisema RC Shigela


Kutoka kulia: Balozi Dkt. Nchimbi (Katibu Mkuu CCM-Taifa) akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela kablasha la kero za wananchi.

Ziara ya katibu mkuu CCM balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi imefanyika katika halmashauri tatu za mkoa wa Geita amabazo ni Chato, Geita DC na Geita TC.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments