Wa kwanza kushoto, Novatus Lyaruu (Katibu wa GPC), wa pili kutoka kushoto, Rodney Thadeus (Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo) anayefuata ni Mwenyekiti wa GPC; Renatus Masuguliko, sambamba na Rose Mweko,mjumbe wa kamati tendaji GPC, wa pili kutoka kulia makamu mwenyekiti, Victor Bariety na katibu msaidizi Ernest Magashi
Jana, tarehe 31 Julai 2024, Mkurugenzi msaidizi wa idara ya habari maelezo, Rodney Thadeus, alitembeea ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC),lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya klabu hiyo na idara ya habari maelezo.
Katika ziara hiyo, Rodney Thadeus, alisema anathamini sana mchango wa klabu ya wandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC) na kutoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kuandika habari za maendeleo yanayofanywa na serikali, lakini pia alionyesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na waandishi wa habari katika kuhabarisha umma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus (wa tatu kutoka kushoto, aliyeweka mikono mbele),akiwa na viongozi wa wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC) .


0 Comments