TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

NELICO YAKABIDHI PIKIPIKI KWA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA GEITA

Na Theresia Method

Shirika  lisilokuwa la kiserikali la new light child organization  (NELICO), chini ya uongozi wa Mkurugenzi Paulina Alex Majogolo, limekabidhi pikipiki kwa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita jana tarehe 6 Agosti 2024 katika ofisi za NELICO mkoani Geita. Pikipiki hiyo inatarajiwa kusaidia kuboresha shughuli za klabu katika kutafuta na kusambaza habari kwa jamii.


Akikabidhi pikipiki hiyo, mkurugenzi wa NELICO amewaomba waandishi wa habari kuendelea kuzifikia jamii na kuibua changamoto zao hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kuzifikia ofisi na taasisi nyingine ili kero zao zifike kwa wakati na kutafutiwa ufumbuzi


Pikipiki hiyo imekabidhiwa  kwa mwenyekiti wa GPC, Renatus Masuguliko, na kueleza kuwa msaada huu utawezesha waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. Alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari katika kuelimisha, kuhamasisha, na kuonya jamii. “Tunatarajia pikipiki hii itarahisisha shughuli za utafutaji habari na kuiwezesha klabu kutimiza majukumu yao kwa ufanisi,” alisema Majogolo. 


Majogolo amesema NELICO itaendelea kushirikiana na GPC kwa kutambua mchango wao muhimu kwa jamii. Amewaomba wadau wengine katika mkoa wa Geita kuunga mkono klabu ya waandishi wa habari kwa kuwa kazi yao ina manufaa kwa jamii yote. "Tuweze kujenga tasnia ya habari mkoani Geita kwa ushirikiano wetu, kwani maendeleo ya Geita yanatokana na juhudi za wana Geita wenyewe," alisema Majogolo



Pichani ni, Mkurugenzi wa NELICO kabla ya kukabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC)


Kwa upande wake, mwenyekiti wa GPC, Renatus Masuguliko, amesema usafiri huo utaongeza kasi ya utendaji kazi hasa katika kuhabarisha umma, kwa niaba ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita , Masuguliko ametoa shukrani za dhati kwa NELICO na kutambua umuhimu wa pikipiki hiyo itakavyosaidia katika shughuli za kiofisi za kuendelea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali hasa ya vijijini. "Pikipiki hii itaboresha utoaji wa taarifa kwa haraka na usahihi, na itatoa dira kwa wadau wengine,” aliongeza Masuguliko.

Makabidhiano hayo yanaashiria hatua nyingine muhimu katika kuimarisha sekta ya habari mkoani Geita.





Mkurugenzi wa NELICO,  Paulia Alex Majogolo akikabidhi funguo za pikipiki kwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Geita(GPC), Renatus Masuguliko.



 

 


Post a Comment

0 Comments