NA EDITHA EDWRD
GEITA 01/8/2014
Naibu Waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama nchini inazidi kuimarika kwa kuongeza ulinzi katika mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi
Naibu waziri, Daniel Sillo ameeleza hayo akiwa safarini mkoani Geita kuelekea Mkoa wa Mwanza akitokea mkoani Kagera, akiwa mkoani humo alipata nafasi ya kusalimiana na viongozi na wadau walioshiriki kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Geita (RCC).
Naibu waziri wa mambo ya ndani, amesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wote wenye vigezo wanapata vitambulisho vya taifa ili kuepuka changamoto ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikijitokeza wanapohitaji huduma mbalimbali sambamba na kudhibiti wahamiaji haramu.
Amewataka viongozi wote wa mkoa wa Geita pamoja na wananchi kuendelea kushirikiana katika kufanikisha zoezi la uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwaka huu uwe wa huru na haki, ili kupata viongozi sahihi wa kuwatumikia wananchi.
Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na kutokuwaa na changamoto za wahamiaji haramu licha ya kuwa ni miongoni mwa mikoa iliyopo pembezoni.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela alisema mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa viongozi wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi watahakikisha uchaguzi huo unafanyika huru na wa haki.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela
MWISHO.
0 Comments