TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

KANISA LA HABARI NJEMA GEITA LATOA ZAWADI NA MSAADA WA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 1 .5 KWA WAFUNGWA NA WAGONJWA

Na Samwel Masunzu-Geita

Jamii mkoani Geita imeaswa kuendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma kwa wananchi ili kufanikisha malengo ya serikali ya kutoa huduma katika jamii

Hayo yameelezwa na askofu Tryphone John wa kanisa la HABARI NJEMA Geita hapo jana septemba 29,2024 baada ya kutembelea gereza la wilaya ya Geita pamoja na hospitali ya mji wa Geita na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa na wagonjwa wakiwemo watoto waliozaliwa kabla ya umri, (njiti) wajawazito na wodi ya watoto ikiwa ni katika kuadhimisha kilele cha wiki ya vijana katika kanisa hilo.

Askofu John amesema wakati serikali ikiendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kujenga shule, kuongeza vyumba vya madarasa, hospitali, vituo vya afya na zahanati, ipo haja ya jamii kuendelea kuunga mkono jitihada hizo za serikali 

"Kwa kutambua jitihada za serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sisi kama kanisa tumeamua kuja kuwaona watu waliopo gerezani pamoja na wagonjwa kwenye hospitali ya mji wa Geita tukiwa na zawadi na misaada mbali ili kurejesha matumaini ya watu hao". alisema Askofu Tryphone John

Mwenyekiti wa vijana kanisa la HABARI NJEMA Geita  Fidel Seluke pamoja pamoaja na Agnes  Moses na Festo  Mgema ambao ni moja wa vijana  walieleza kuwa  mara kadhaa wamekuwa wakifanya hivyo kwa kushiriki huduma nyingine ikiwemo za kuchangia damu.

Hata hivyo wito ulitolewa   kwa jamii juu ya kuwaona wafungwa na wagonjwa katika nyakati wanazozipitia, 

Wito huo ulitolewa na  kaimu mkuu wa gereza wilaya ya Geita, mrakibu msaidizi wa jeshi la magereza Samwel Juma na daktari Dickson Magezi kutoka hospitali ya mji Geita baada ya kupokea zawadi na misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1 na laki 5 ambavyo ni magodoro, sabuni, mafuta , sukari, maji na juisi.

Askofu Tryphone John mwenye suti akikabidhi msaada wa vitu kwa kaimu mkuu wa gereza la wilaya ya Geita.



Askofu Tryphone John akiwa wodini akiwaombea wagonjwa kwenye wodi ya watoto.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments