Na Samwel Masunzu-Geita,
Mwenge wa uhuru wa mwaka 2024 umewasili mkoani Geita ambapo utakimbizwa mkoani humo kuanzia leo septemba 30 hadi oktoba 5, 2024.
Mwenge huo umepokelewa mkoani Geita na mkuu wa mkoa wa Geita Mhe: Martine Shigela katika wilaya ya Chato ukitokea mkoa wa Kagera
Mwenge ukiwa mkoani Geita utakimbizwa kilomita 826.6 na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi 18, kuzindua miradi 22, kutembelea na kuona miradi 25 yenye thamani ya shilingi bilioni 32.2
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe: Martine Shigela baada ya kupokea mwenge huo ameukabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Chato Louis Peter Bura na jumla ya miradi 10 itapitiwa katika wilaya hiyo
Mkesha wa mwenge wa uhuru baada ya kukamilisha ratiba ya kukagua nakupitia miradi ya maendeeleo utafanyika katika kata ya Buseresere wilaya ya Chato
Kauli mbiu ya mwenge wa mwaka 2024 ni “Tunza mazingira, shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu"
Mwisho

0 Comments