Na Samwel Masunzu,
Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Mkoa wa Geita umewataka vijana kuepuka kutumiwa na baadhi ya makundi katika kuchafua amani nchini, badala yake wailinde amani ambayo ni tunu iliyoasisiwa na viongozi waliotangulia kwa manufaa ya vizazi vya baadae
Mwenyekti wa UVCCM mkoa wa Geita Manjale Magambo ameeleza hayo wakati akifunga makambi ya vijana ambayo yamefanyika kwenye kata ya Buseresere wilayani Chato, na kwamba vijana ndiyo wanapaswa kuwa msatari wa mbele na kuepuka kutumiwa na baadhi ya makundi katika kuchafua amani ya nchi
Wakati huo huo, ilielezwa kuwa ili kupata viongozi watao kuwa chachu ya kuleta mabadiriko chanya katika jamii, makundi mbalimbali yakiwemo ya vijana na wanawake yapaswa kujiandikisha katika daftari la makakazi ili kupata sifa za kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ambao ni wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.
Rai hiyo ilitolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’whale mkoani Geita Husna Tony kupitia mikutano ya hadhara ya mbunge wa jimbo la Nyang’whale Mhe. Hussein Kassu
Aidha Husna Tony alieleza kuwa, walioboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura hawatakuwa na sifa za kuchagua viongozi wa vijiji na mitaa ispokuwa madiwani, wabunge na Rais na hii ni endapo hawatakuwa wamejianidikisha katika daftari la makazi
Ikumbukwe kuwa tarehe 11 hadi 20 mwezi wa 10 ni tarehe ya kujiandikisha kwa wapiga kura, tarehe 21 mwezi wa 10 ni tarehe ya kubandika orodha ya wapigakura, tarehe 25 mwezi wa 10 ni tarehe ya ukomo wa viongozi waliopo madarakani, taereh 1 hadi 7 mwezi wa 11 itakuwa ni tarehe ya kuchukua fomu na kurudisha fomu za wagombea, tarehe 20 hadi 26 mwezi 11 itakuwa tarehe ya kuanza kwa kampeni na terehe 27 mwezi wa 11 ndipo utafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa huku ukisubriwa uchaguzi mkuu wa mwakani 2025 wa kuwapata madiwani, wabunge na Rais.
Mwisho.
.jpg)

0 Comments