Na Victor Bariety;
Katika historia ya kisasa ya
Tanzania, michezo imeendelea kuwa zaidi ya burudani. Imegeuka kuwa jukwaa la
mshikamano, siasa, na dira ya maendeleo ya jamii. Hili lilidhihirika wazi
katika mkutano uliofanyika Nyankumbu, Geita, ambapo wanachama wa Tawi la Yanga
Nyankumbu Senta “Mpaka Waseme” walijumuika kwa pamoja, si kwa ajili ya
kushangilia ushindi wa timu yao pekee, bali kwa kauli moja kuahidi kura zao kwa
Rais Samia Suluhu Hassan na wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Risala ya Mshikamano na Maendeleo
Katibu Mkuu wa tawi hilo, Goodluck Godwin Pambe, amemama mbele ya wanachama na wageni waalikwa kusoma risala iliyojaa uhalisia. Risala hiyo ilionyesha safari ya tawi, kuanzia kuanzishwa kwake tarehe 30 Julai 2025 na wanachama 32 tu, hadi kufikia wanachama 90 walio hai kwa sasa.
Wanachama hao walijitolea fedha
kidogo walizokuwa nazo – kiingilio cha shilingi 1,000 na mchango wa shilingi
5,000 kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa kumbukumbu. Hadi sasa wamekusanya zaidi
ya shilingi 600,000 ambazo zimewezesha kuanza ujenzi wa mnara huo, ingawa bado
unahitaji kukamilishwa.
Changamoto zimebaki: uhitaji wa
shilingi 500,000 kukamilisha taa, tofali, bomba na nyavu. Aidha, mipango ya
baadaye ni makubwa zaidi – ununuzi wa viti 200, matenti matano, pamoja na
vyombo vya kijamii vya matumizi ya pamoja, mradi wenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 16.5.
Kwa hakika, risala hii haikuwa
maelezo ya fedha pekee, bali ni taswira ya mshikamano na dira ya maendeleo ya
kijamii.
Mgeni Rasmi Atoa Ahadi
Mhandisi Chacha Mwita Wambura, mgombea ubunge wa CCM jimbo la Geita mjini, alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo. Akiguswa na mshikamano wa wanachama, alisema kwa tahadhari:
“Nimesikia risala yenu na
ninaahidi kuwashika mkono mara baada ya kushinda ubunge. Kwa sasa nikifanya hivyo
inaweza kutafsiriwa vibaya kama rushwa, lakini baada ya ushindi mtashuhudia
matunda ya mshirikiano wetu.”
Kauli hii ilipokewa kwa shangwe
kubwa, ikionyesha imani kwamba wanayanga wa Nyankumbu si tu mashabiki wa mpira,
bali pia ni raia wenye uelewa wa kisiasa.
Goli la Mama: Mchango wa Samia Katika
Michezo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Mhoja Mapande, aliweka bayana kile ambacho wanayanga wengi wameshuhudia kwa macho yao – mchango wa Rais Samia katika michezo.
“Goli la Mama limeipeleka
michezo hatua ya juu sana. Ndiyo maana Yanga na Simba waliweza kucheza fainali
ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa nguvu hii, hakuna shaka Oktoba tutamtiki
Mama Samia, Mbunge wetu Chacha na Diwani wetu Sukambi.”
Kauli hii ni zaidi ya siasa. Ni
uthibitisho kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia, michezo imepata
uangalizi na uwekezaji wa aina yake. Soka la Tanzania limeanza kushindana
kimataifa, na vilabu vikubwa kama Yanga na Simba vimevuka mipaka ya ukanda huu
na kuonyesha ubora wa kipekee.
“Goli la Mama” si neno la mzaha. Ni kauli inayobeba historia ya namna Rais Samia alivyoamua kusimama mstari wa mbele kuwekeza katika michezo kama dira ya kitaifa.
Kura kwa Michezo, Kura kwa Maendeleo
Katika shangwe za wanayanga, sauti moja ilisikika:
“Tunatiki kwa Mama! Tunatiki kwa
Mbunge! Tunatiki kwa Diwani! Wapinzani mpaka wasemeee!”
Kauli hii ni ya kisiasa, lakini imefungwa kwa vitendo vya maendeleo. Wanachama wa Nyankumbu wameona kwa macho yao jinsi serikali ya Rais Samia imeleta mageuzi: miundombinu ya viwanja, uwezeshaji wa timu, na dira ya michezo kuwa ajira rasmi kwa vijana.
Katika mantiki hiyo, kura kwa Rais
Samia si kura ya chama pekee, bali ni kura ya kuendeleza michezo na maendeleo
ya jamii kwa ujumla.
Mwenyekiti wa tawi la Yanga
Nyankumbu, Hassan Mshola (maarufu Mwibara), alihakikisha kwa kauli thabiti kuwa
hawana shaka na mwelekeo wao wa kisiasa.
“Sisi wanachama wa tawi hili
tumeona juhudi za Mama kwenye michezo, hasa hili ‘Goli la Mama’. Tumepanga kuhakikisha
Rais Samia, Mbunge na Diwani wanapata kura nyingi. Yanga mbele, CCM mbele,
Nyankumbu mbele.”
Hii ilikuwa ni sauti ya msingi –
ishara kuwa siasa inatoka chini kwenda juu, kwa wananchi wenyewe.
Uchambuzi: Michezo Kama Dira ya Kura
Tukio la Nyankumbu linafungua mjadala mpana kuhusu nafasi ya michezo katika siasa. Kwa muda mrefu, mpira wa miguu umejulikana kama burudani ya wanyonge, lakini sasa umekuwa daraja la mshikamano na dira ya kitaifa.
Kwanini wanayanga Nyankumbu wamesema kura zote kwa Mama Samia? Jibu lipo kwenye uhalisia:
1. Uwekezaji wa Serikali: Samia ameingia na kubadilisha taswira ya michezo, kutoka burudani hadi uchumi.
2. Mafanikio ya Vilabu: Ushiriki wa Yanga na Simba katika mashindano ya CAF ni ushahidi wa kimataifa.
3. Ajira kwa Vijana: Michezo imeanza kuajiri maelfu ya vijana, jambo linalopunguza ukosefu wa ajira.
4. Taswira ya Nchi: Tanzania sasa inatajwa kwenye ramani ya michezo barani Afrika.
Kwa uchambuzi huu, kura za Nyankumbu kwa Mama Samia si za kishabiki tu, bali ni za kimkakati kwa maendeleo.
Hitimisho
Michezo ni maisha, na maisha ni
siasa. Wanayanga Nyankumbu wameandika ukurasa mpya kwa kuunganisha yote mawili.
Kwa risala yao, ahadi zao na mshikamano wao, wamesema wazi: Oktoba 29 hawana
shaka – kura zote ni kwa Rais Samia Suluhu Hassan na wagombea wa CCM.
Kwao, “Goli la Mama” si kumbukumbu ya
uwanjani tu, bali ni dira ya kitaifa ya mshikamano na maendeleo.
Imeandaliwa na Victor Bariety – 0757-856284




















0 Comments