Na Mwandishi wetu;
Mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda
kwa tiketi ya CCM, Dkt. Jafari Rajabu Seif, leo Septemba 1, 2025, ameshiriki
katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru uliopokelewa rasmi leo Mkoani Geita.
Shughuli hiyo imefanyika katika
Kijiji cha Rwezera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ikiwa ni sehemu ya mapokezi
ya mbio hizo zitakazodumu mkoani humo hadi Septemba 6, 2025.
Katika mbio hizo, Mwenge wa Uhuru
unatarajiwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali
ya maendeleo inayofikia jumla ya miradi 61, yenye thamani ya takriban shilingi
bilioni 164.Dkt. Jafari amepongeza jitihada za
serikali katika kusimamia maendeleo na kuahidi kushirikiana kwa karibu na
wananchi wa Jimbo la Busanda katika kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa
jamii.
0 Comments