TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM SENGEREMA IMEADHIMISHA MIAKA 46 YA KUZALIWA CCM KWA KUWAFUTA MACHOZI WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NA KUPANDA MITI 500

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  JAckson Mazinzi akikabidhi taulo za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyampulukano. 


Anna Ruhasha, Mwanza.

Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM ), Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema Mkoani Mwanza imetoa msaada wa taulo za kike na madaftari kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu katika shule ya Sekondari  Nyampulukano pamoja na kupanda miti mia tano (500) katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  JAckson Mazinzi akikabidhi daftari kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyampulukano. 

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wanafunzi wa shule hiyo  Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Sengerema Jackson Mazinzi  amesema kuwa Jumuiya hiyo imetoa vifaa hivyo ili kuwasaidia  wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki, na kuwaagiza walimu wa shule hiyo kusimamia kikamilifu miti hiyo 500 ili iweze kukua.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Jackson Mazinzi akiongoza zoezi la kupanda miti ili kutunza mazingira katika shule ya sekondari Nyampulukano. 

Baadhi  ya Wanafunzi wa shule hiyo walio pewa misaada hiyo wameishukuru Jumuiya  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapatia vifaa kwa kuwa vitawasaidia kusoma katika mazingira rafiki.

Picha ya baadhi ya Wanajumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  wakiadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa CCM kwa kupanda miti ili kutunza mazingira katika shule ya Sekondari Nyampulukano Wilayani Sengerema. 

Naye makamu mkuu  wa shule ya Sekondari Nyampulukano Maemba Katemba ameipongeza Jumuiya hiyo kwa kupanda  miti 500 katika shule hiyo na kutoa misaada hiyo kwa wanafunzi. 

Baadhi ya Wanajumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi na Wanafunzi  wakiadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa CCM kwa kupanda miti ili kutunza mazingira katika shule ya Sekondari Nyampulukano Wilayani Sengerema.

Awali  katibu  wa Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha  Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema Jamal Twalib Athuman amewashukuru viongozi  wa Jumuiya hiyo kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki zoezi hilo la upandaji miti na utoaji wa msaada wa vifaa hivyo muhimu kwa Wanafunzi wa kike wawapo shuleni.

Jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Sengerema wameadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM kwa zoezi la kupanda miti 500 na kugawa taulo za kike kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyampulukano Sengerema Mwanza. 


Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments