Na mwandishi wetu;
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Nikolaus Kasendamila, amewataka wagombea na wanachama wa chama hicho waliokuwa wakihusishwa na mchakato wa kuwania nafasi za udiwani katika Jimbo la Busanda kuweka pembeni makovu na vinyongo vilivyotokana na kura za maoni, na kuelekeza nguvu katika kutafuta kura za ushindi kwa wagombea wa CCM.Akizungumza katika kikao maalum kilichofanyika kata ya Nyarugusu, Kasendamila amesema anakiri kuwepo kwa mikwaruzano na mipashano miongoni mwa wanachama wakati wa mchakato wa ndani wa uteuzi, lakini akasisitiza kuwa sasa ni wakati wa umoja na mshikamano ili kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo.
"Ninatambua kulikuwa na
sintofahamu na mikwaruzano kwenye baadhi ya kata, lakini hayo yamepita.
Tunachotakiwa sasa ni kuelekeza nguvu zetu kwenye kutafuta kura kwa wagombea wa
CCM madiwani, mbunge, na mgombea urais Dkt. Samia Suluhu Hassan,"
amesema Kasendamila.










0 Comments