TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

NGELEJA ADAIWA KUWANUSURU WANAFUNZI WAKIKE KUWEKWA VIMADA NA KUWEKWA NYUMBA NDOGO.


Na Renatus Masuguliko-Sengerema;


Picha: Mzee Sangija Nguno Mwenyekiti mstaafu wa  serikali ya kijiji cha Bitoto wilayani Sengerema mkoani Mwanza, ambaye pia ni mdau wa elimu anayesema mchango wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo William Mganga Ngeleja kati ya mwaka 2005 hadi 2020 unastahili kuenziwa.

Wakazi wa kata ya Bitoto wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamesema kuwa  hatua ya aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Sengerema William Mganga Ngeleja  ya    kuwajengea shule ya sekondari kwa fedha yake imegeuka chachu  ya elimu katika kata hiyo.

Imedaiwa kuwa hatua hiyo  imewanusuru  watoto wa kike kutowekwa vimada,  wengine kufanywa nyumba ndogo na kuolewa kutokana na awali kulazimika kupanga mitaani kutokana na shule kuwa mbali.

Kutokana na kuwepo kwa hatua hiyo baadhi ya wadau wa maendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu wameomba kuhuishwa kwa mchakato wa awali uliokuwepo wa kutaka  kumuenzi kwa shule hiyo kupewa jina lake hatua itakayowatia moyo pia wadau wengine katika kuchangia shughuli za kijamii  za maendeleo.

Mwenyekiti mstaafu wa serkali ya kijiji cha Bitoto Sangija Nguno aliyesimamia na kuratibu ujenzi wa sekondari hiyo amesema jana kijijini hapo kuwa fedha iliyotumika kujenga sekondari hiyo ni ya Ngeleja binafsi na yeye ndiye aliyekuwa mratibu na msimamizi  mkuu wa ujenzi huo ulioanza mwaka 2017 na kukamilika na kuanza kupokea wanafunzi toka mwaka  2010.

Nguno ambaye amekuwa mwenyekiti wa serkali ya kijiji cha Bitoto kwa zaidi ya miaka 20 anadai kuwa huo ulikuwa ni mkakati wa Ngeleja  wa kuwaondolea kero wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na sekondari wa kiwemo wa kike kusafiri umbali wa kati ya kilometa   20 kwenda na kurudi.

Ili kuunga mkono juhudi zake, Jamii ilibuni utaratibu wa kuhakikisha kila mzazi anayesaidia au kushiriki kukatisha masomo ya mtoto  wakike kwa lengo la kumuozesha kuhakikisha  anaadhibiwa na jamii na kila mwanajamii ni mlinzi wa mtoto wakike   utaratibu ambao umekuwa chachu katika jimbo la Sengerema na kuzaa matunda yaliyokusudiwa.

“Uwekezaji alioufanya Ngeleja kwa kujenga sekondari hiyo hautasahaulika, kwani unaendana na maono ya   Rais Samia Suluhu  Hassan anayoyahubiri sasa ya kuhakikisha  elimu  kwa mtoto  wa kike inapewa kipaumbele” alisema Mzee Nguno.

Kutokana na sekondari kuwepo umbali mrefu hatua hiyo ndiyo  iliyowalazimisha  wanafunzi wakiwemo wakike kupanga mitaani ambako baadhi yao walifanywa vimada, nyumba ndogo na kuolewa hivyo kukatisha ndoto zao za masomo.

Kabla ya kujengwa kwa sekondari hiyo ambayo awali wananchi waliomba ipewe jina la Ngeleja lakini Ngeleja mwenyewe alikataa kuitwa kwa jina lake lakini kwa sasa wananchi wanadai wanaomba mchakato huo wa kumuenzi kwa kuiita shule sekondari hiyo jina lake uhuishwe upya.

Wanatetea hatua hiyo kutokana na mchango wake huo, ambao umeonesha kuwa msaada mkubwa na chachu ya elimu katika kata na jimbo la Sengerema kwa kupunguza umbali wa kutembea kati ya kilometa kumi kufikia shule jirani za sekondari  zikiwemo za Buyagu na Ngoma sekondari lakini sasa  wanatembea umbali wa kati ya kilometa  sufuri hadi kilometa mbili tu kufika shule hivyo kuwatia moyo kutimiza  ndoto zao.

Dotto Maguzu mmoja wa wadau wa Elimu na maendeleo katika kata ya Bitoto anasema kuwa hatua hiyo inastahili kupongezwa na kumuenzi kwa  wananchi  wanahakikisha kila mtoto wakike anayefaulu kujiunga na sekondari anatimiza ndoto yake kwa jamii kuweka utaratibu wa kumbana kila mzazi kuhakikisha anawajibika kuanzia ngazi ya familia hadi jamii.

Wanafunzi Martha  Peter anayesoma kidato cha tatu katika sekondari ya Bitoto na Herena Musa anayesoma kidato cha kwanza katika sekondari ya Bitoto  wanasema kuwa uwepo wa sekondari hiyo umegeuka  chachu kwa wanafunzi hasa wa kike kutimiza ndoto zao ikilinganishwa na wenzao waliowatangulia.

“Kwa sasa hakuna mwanya  tena wa  kusingizia  kukwepa kufika sekondari wakati ule wenzetu waliotutangulia walikumbana na vishawishi vingi njiani, ikiwemo kuishia kuolewa na kupewa ujauzito  kutokana na kulazimika kusafiri umbali mrefu na mara nyingine kupanga mitaani” alidai Martha

Kwa upande wake Herema anayesoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Bitoto anasema kuwa kwa sasa wasichana wamehamasika kutimiza  ndoto zao bila kusahau  kumshukuru aliyetumia rasimali zake kujenga sekondari hiyo ili kumuenzi wanafunzi wa kike wamedai watamuenzi  kwa kusoma kwa bidii ili kutimiza  ndoto zao.

Awali Kabla ya kujengwa  sekondari ya Bitoto Wanafunzi kutoka vijiji ikiwemo kata ya  Bitoto walikuwa wanalazmika kufuata sekondari katika kata jirani za Buyagu na Ngoma umbali wa zaidi kilometa  ishirini kwenda na kurudi hatua iliyowalazimisha wanafunzi kupanga vyumba mitaani ili wawepo karibu na shule hatua iliyochangia baadhi kukatisha masomo na utoro.

William Mganga Ngeleja aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la sengerema kutoka mwaka 2005 hadi 2020 alipotakiwa kuzungumzia hatua ya yeye kukataa kwa sekondari hiyo kuitwa jina lake amesema ilikuwa ni mapema mno kufanya hivyo.

Hata  hivyo Ngeleja amesema hana kizuizi cha kuzuia maamzi ya wananachi ambao ndio wadau wa maendeelao kutimiza  adhima yao kwani yeye baada ya kukamilisha ujenzi huo aliikabidhi kwa mamlaka husika na lengo lake kubwa lilikuwa kumaliza  kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wanaochaguliwa kujiunga na sekondari hasa  wasichana kwani wengi wao walikuwa wanakatisha  kumaliza  masomo kutokana na umbali.

Mwisho.

 

 

Post a Comment

0 Comments