TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

INAWEZEKANA KUTOKUWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KATIKA MJI WETU WA GEITA

 

Waumini wa kanisa la The voice Of  Gospel wakifanya Usafi.

Taasisi , makampuni mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi Mjini Geita wameshauriwa kuzingatia usafi wa mazingira hususani katika kipindi hiki cha msimu wa mvua ili kukabiliana na changamoto ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Rai hiyo imetolewa na Mchungaji wa kanisa la The Voice Of Gospel Inaternational Ministrie Chamos Polepole wakati wa zoezi la kufanya usafi katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu ikiwemo katika masoko ya Mbagala na Nyankumbu mjini Geita.


Amesema kanisa hilo limejenga tabia ya kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo ya umma kama hosptali kwakuwa maeneo hayo nimuhimu na yanamuingiliano mkubwa wa watu,nakutumia fursa hiyo kuwashauri watu wengine , taasisi na makampuni mbalimbali kuona umuhuhimu wa kushiriki usafi katika maeneo umma.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Geita Mwenyekiti wa soko la Mbagala mjini Geita amepongeza hatua ya uongozi wa kanisa hilo kujitokeza mara kwa mara kufanya usafi katika eneo hilo,nakusema kuwa hatua hiyo itasaidia wafanyabiashara katika eneo hilo kufanya kazi zao kwa kujiamini na bila kuwa na hofu ya magonjwa ya mlipuko.

 

 


Post a Comment

0 Comments