![]() |
Mhe. Kanali Michael Mntenjele Mkuu wa wilaya Tandahimba akifungua mkutano mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Tandahimba leo 20.03.2025 |
Na: Beatus Bihigi - Mtwara.
Mhe. Kanali Mntenjele amewataka walimu kuzingatia maadili yao ya kazi na kujiepusha na vitendo visivyo faa katika jamii wanazoishi na kufanya kazi" Walimu tunaaminiwa hivyo tuwe mfano kwa kila jambo ikiwemo uvaaji wenu, haifai Mwalimu kuvaa kata kundu yaani K. K" alisema Kanali Mntenjele Mkuu wa wilaya Tandahimba.
![]() |
Mhe. Kanali Michael Mntenjele (Mkuu wa wilaya Tandahimba) aliyesimama akifungua mkutano Mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Tandahimba leo 20/03/2025 |
![]() |
Mhe. Kanali Michael Mntenjele (Mkuu wa wilaya Tandahimba) aliyesimama akifungua mkutano Mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Tandahimba 20 March 2025 |
![]() |
Mhe. Kanali Michael Mntenjele (Mkuu wa wilaya Tandahimba) aliyesimama akifungua mkutano Mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Tandahimba. |
Aidha Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe. Kanali Michael Mntenjele amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwafundisha Wanafunzi katika shule za msingi na sekondari maeneo yote ya Wilaya ya Tandahimba.
![]() |
Pichani ni Deogratiasi Hokororo - Katibu msaidizi tume ya utumishi wa walimu (TSC) Wilaya ya Tandahimba. |
![]() |
Pichani kushoto ni Rajabu Saidi -Kaimu Afisa Elimu awali na msingi wilaya ya Tandahimba na kulia ni Mzunza hazina mstaafu CWT wilaya ya Tandahimba Mwl. Rajabu Nalola |
Pamoja na mambo mengine aliyotolea ufafanuzi kwa ngazi ya Wilaya Mhe Kanali Mntenjele amewaahidi walimu Ofisi yake kuendelea kushirikiana na Chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Tandahimba.
Chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Tandahimba kimefanya mkutano Mkuu wake leo tarehe 20/03/2025 ukiwa na ajenda zisizopungua nane lakini kuu ikiwa ni ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho ngazi ya Wilaya.
Mwisho
0 Comments