TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

"MNDUMBWE SEKONDARI TUKO VIZURI" NTARISA K. NTARISA

Ntarisa K. Ntarisa - Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe wilayani Tandahimba - Mtwara 

Na. Beatus Bihigi - Mtwara.
Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe iliyopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara Mwalimu Ntarisa K. Ntarisa akiwa  katika furaha amewapongeza walimu wa michezo katika shule hiyo kufuatia ushindi walioupata dhidi ya shule ya sekondari Milongodi mwishoni mwajuma tarehe 28 February 2025.
Ramadhani Salum Migeto - Makamu Mkuu wa Shule ya sekondari Mndumbwe akitoa nasaha zake kwa Wanafunzi kabla ya mashindano ya michezo mbali mbali kuanza. 

Shule ya sekondari Mndumbwe waliwakaribisha shule ya sekondari Milongodi katika mashindano ya kirafiki, ambapo walishindana katika mdahalo (Debate) kwa lugha ya Kiingereza na Mndumbwe sekondari kuibuka mshindi.
Aidha katika mchezo wa mpira wa miguu Mndumbwe sekondari waliibuka kidedea kwa kuwabamiza goli mbili kwa moja timu ya mpira wa miguu ya Milongodi.
Wanafunzi meza kuu wakiwa kwenye mdahalo/ debate leo tarehe 28/2/2

Wanafunzi wakiwa katika mdahalo shule ya sekondari Mndumbwe 28 February 2025

Wanafunzi wa Milongodi wakiwa wameketi mbele wakati wa mdahalo na wenzao Mndumbwe waliovalia t-shirts za kijani. 

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mndumbwe na wageni wao kutoka shule ya sekondari Milongodi wakiwa kwenye debate 28/2/2025

Kwaupande mwingine katika mpira wa mikono yaani netball Shule ya sekondari Mndumbwe iliendeleza ubabe kwa kuwafunga shule ya sekondari Milongodi goli 18 kwa 4 Milongodi. 

Aidha michezo hujenga afya na kuondoa changamoto ya utoro shuleni hali inayopelekea kupanda kwa ufaulu wa masomo kwa Wanafunzi na shule kwa ujumla. 
Pichani waliosimama mbele ni walimu , upande wa kushoto ni kutoka Milongodi na kulia ni kutoka Mndumbwe, waliochuchumaa ni wachezaji wa timu ya Milongodi na waliosimama ni timu ya Mndumbwe sekondari. 

Wachezaji wa netball wa Milongodi sekondari (waliosimama) na Mndumbwe sekondari ( waliochuchumaa ) 28/2/2025

Mwalimu kutoka shule ya sekondari Milongodi wilayani Tandahimba mkoani Mtwara akipata chakula Mndumbwe sekondari akisubiri Wanafunzi kushindana katika mchezo wa mpira wa miguu. 

Mwalimu Hamza, Mwalimu wa somo la Elimu ya dini ya kiislamu katika shule ya sekondari Mndumbwe 

Wakwanza kulia ni Ntarisa K. Ntarisa Mkuu wa shule ya sekondari Mndumbwe akiwa na baadhi ya walimu kutoka Mndumbwe na Milongodi 

Wapili kutoka kulia ni Dativa Paul (Afisa maendeleo ya jamii kata ya Mndumbwe akipata chakula cha pamoja na walimu kutoka Milongodi waliofika katika shule ya sekondari Mndumbwe kwaajili ya michezo. 


Madam Mwansite Wiliard Shali (Mwalimu wa michezo katika shule ya sekondari Mndumbwe Tandahimba. 

Sir. Gabriel Shirima Valentini (Mwalimu wa kemia na miradi Mndumbwe sekondari) akifurahia ugeni wa shule jirani ya Milongodi kuwatembelea kwaajili ya michezo 

Mathayo Michael Kwaslema (Mwalimu wa taaluma katika shule ya sekondari Mndumbwe) akiwa mwenye furaha.




Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments