Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewatahadhalisha watumishi wazembe na wanaotoa lugha chafu kwa wagonjwa kuwa hawatavumiliwa kwa kuwa kwa kufanya hivyo nikukiuka sheria za utumishi.
Ametoa kauli hiyo Desemba 03, Mwaka huu katika kikao kilichowakutanisha wadau wa Afya na Elimu Mkoani Geita katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliyopo halmashauri ya Mji wa Geita nakuwakumbusha wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kuwa yamekuwa tishio hapa nchini.
Akiwa katika kikao hicho Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dakta Japhet Simeo amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za utumishi Ili kuepuka migogoro na serikali nakumhakikishia Mganga mkuu wa serikali kuwa atahakikisha watumishi wazembe katika mkoa huo hawatavumiliwa.
Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandis Robert Gabriel ambae alikuwa Mgeni rasmi katika kikao hicho
amewataka watumishi wa Afya na Elimu Mkoani Geita kutimiza majukumu yao bila
kusukumwa kwakuwa uongozi siyo starehe.
Wadau wa Afya Mkoani Geita wakiwa katika kikao cha pamoja
0 Comments