Mkuu wa wilaya ya Chato Mkoani Geita Mhandis
Charles Kabeho amefuta likizo zote kwa watumishi wa serikali katika wilaya hiyo,
nakuwaagiza kutumia kipindi cha mwezi mmoja kufanya ukamilifu wa ujenzi wa vyoo
na madarasa yaliyo katika hatua ya mwisho, kabla ya shule kufunguliwa mwaka
kesho.
Akizungumza katika uzinduzi wa baraza la madiwani wilayani humo Desemba 11, katika ukumbi wa shule ya sekondari Chato Mhandis Charles kabeho amesema, ili kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wilayani humo, nivyema kila Mtumishi wa serikali akawajibika kwa nafasi yake bila kusukumwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Eliud
Mwaiteleke amewatahadharisha watumishi wazembe katika eneo hilo kuwa waanze kujiengua mapema
kwani awamu hii haihitaji watumishi wavivu.
Baadhi ya madiwani walioapishwa wamempongeza Mkuu wa wilaya ya Chato kwa hatua ya kufuta likizo zote kwa watumishi wa umma, kwani itasaidia kupunguza changamoto katika shule za msingi na sekondari kwa muda mchache uliosalia.
Akifunga kikao cha baraza hilo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Christian Manunga amewataka watumishi wa umma na madiwani walioapishwa kushirikiana kwa pamoja ili kuwaletea maendeleo wananchi.
0 Comments