TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI AJILIPA MSHAHARA FEDHA YA ELIMU BILA MALIPO

 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita Leonidas Felix alie Kushoto, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandis Charles Kabeho katika zoezi la kukabidhiana vifaa vya kujifunzia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Geita imefanikiwa kurejeshea kiasi cha zaidi ya Shilingi milioni tano kilichokuwa kimefanyiwa ubadhilifu kutoka katika fedha za elimu bila malipo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni iliyopo wilayani chato Mkoani Geita. 

Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita Leonidas Felix akiwa katika hafla ya kumkabidhi Mkuu wa wilaya ya Chato madawati 42, vifaa vya kujifunzia wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwemo photocopy mashine,laptop na projecta kutokana na fedha hizo kuelekezwa kununua vifaa hivyo ili kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.


Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandis Charles Kabeho  katika shule hiyo ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya nakuwataka watumishi wa umma wilayani humo kufanya kazi kwa kwa weledi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Bw Philip Shon amesema atashirikiana na idara ya elimu kufanya uchunguzi kwa shule zote za msingi ili kujiridhisha matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya elimu bila malipo.


 

Post a Comment

0 Comments