Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara ametoa amewataka watendaji wa serikali Mkoani Geita kuhakikisha wanasimamia kwa uwezo wao suala la usafi wa mazingira ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayoweza kujitokeza.
Mhe,
Waitara akiwa katika ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya Mji wa Geita
Mkoani Geita Desemba 28,2020 ametoa
maagizo hayo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita nakusema kuwa viongozi wengi
nchini wamekuwa wakijisahau kusimamia majukumu yao nakusema kuwa suala la usafi
wa mazingira nikila siku nasiyo kila mwisho wa mwezi kama ilivyokuwa.
Kwa upande wake Afisa usafi na mazingira wa halmashauri ya mji wa Geita Bw Aloys Mutayuga amemhakikishia naibu waziri kuwa ataendelea kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kwa uwezo wake wote ili kuepukana na changamoto ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel ameiomba wizara ya mazingira kupitia
kwa naibu waziri Mhe, Waitara kuendelea kushirikiana kwa pamoja na ofisi yake
ili kudhibidi visababishi vya magonjwa ya mlipuko mkoani Geita kwakuwa shughuli
nyingi za wakazi wa eneo hilo ni uchimbaji wa madini uya dhahabu ambao unatumia
kemikali ambazo ni hatari kwa usalama wa maisha ya watu kama zisipo hifadhiwa
vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel
Wananchi
Mkoani Geita wamepongeza hatua ya Naibu waziri kwa kuendelekea kuhimiza suala
la usafi wa mazingira kwakuwa idadi kubwa ya watu nanajisahau sana katika suala
la usafi wa mazingira ikiwemo kujenga nakutumia vyoo bora katika makazi na
maeneo ya biashara zao.
0 Comments