Shirika la Ndege Tanzania ATCL limepanga kuanza safari zake katika Mkoa wa Geita hivi karibuni kufuatia uwanja wa Ndege wa Chato kuwa katika hatua ya mwisho ya matengenezo.
Mtendaji wa shirika la ndege Tanzania ATCL Ladslaus Matind akizungumzia kuanza kwa huduma za usafiri wa anga mkoani Geita.
Akizungumza katika Mkutano wa wakuu wa taasisi mbalimbali kuhusu uanzishwaji wa huduma za usafiri wa anga Mkoani Geita katika ukumbi wa mikutano wa JS Hotel mjini Chato Mtendaji Mkuu wa shirika la Ndege Tanzania ATCL Ladslaus Matindi amesema, ni Mkakati wa serikali kuendelea kujenga viwanja vya Ndege kila mkoa, nakwamba huduma hiyo Mkoani Geita inatarajia kuanza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa matengenezo madogo ya muhimu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel ambae alikuwa Mgeni rasmi katika Mkutano huo amesema kuanza kwa huduma za usafiri wa anga Mkoani Geita kutachangia mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,mifugo,uvuvi madini na utalii.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Haroun Senkuku akitoa taarifa fupi kuhusu mwenendo wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita.
Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandis Charles Kabeho akiwa katika Mkutano na wadau wa taasisi mbalimbali kuhusu ufunguzi wa safari katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita
Mkaguzi Mkuu kiongozi wa viwanja vya ndege tanzania Mhandis Bernard Kavishe akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita namna uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita utakavyo fanya kazi
Muonekano wa sehemu ya kupaki ndege baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita ambao upo katika hatua ya mwisho ya matengenezo
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel akiwa katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Geita na wadau kutoka taasisi mbalimbali.
0 Comments