TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

TAKUKURU MKOA WA GEITA YAREJESHA FEDHA ZA MWALIMU ALIZOKUWA AMETAPELIWA NA MTANDAO WA QNET

Mwalimu Rose Frank akipokea fedha aliyokuwa ametapeliwa na Mtandao wa QNET

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Geita imefanikiwa kumrejeshea Mwalimu wa shule ya Msingi Lukalanga kiasi cha zaidi ya Shilingi milioni tano alichokuwa ametapeliwa na Mtandao wa QNET.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita Leonidas Felix akimkabidhi fedha zake Mwalimu Rose

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake  Mkuu wa  taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa  Geita Leonidas Felix amesema wamefanikiwa kurejesha kiasi chote cha Shilingi Milioni 5,480,000, kwa Mwalimu Rose Frank wa shule ya Msingi lukalanga iliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita baada ya kurubuniwa nakuahidiwa kutengeneza fedha zaidi marudufu na Mtandao wa QNET uliyo na ofisi zake mjini Geita. 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita Leonidas Felix

Katika hatua nyingine Bw Leonidas amesema wamefanikiwa kukamata Box 19 za viuatilifu aina ya DUDUBA EC 450 zilizokuwa zimetolewa na bodi ya Pamba kwa ruzuku ya serikali kwa ajili ya wakulima wa Pamba wa AMCOS ya Bukaga inayojumuisha vijiji vya Bulela na Gamashi zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 9.

Mwakilishi wa Bodi ya Pamba wilaya ya Geita katikati akikabidhiwa viuatilifu aina ya DDUBA

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa dawa hizo mwakilishi wa Bodi ya Pamba wilaya ya Geita na wajumbe wa AMCOS hiyo wameipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya, huku Mwalimu alierejeshewa fedha zake amewaomba watu wengine kujitokeza bila woga kuripoti vitendo vya Rushwa ili viweze kukomeshwa.


Mkuu wa Takukuru mkoani Geita Leonidas akamaliza kwa kutoa Wito wa wananchi pamoja na watumishi wa umma, kuendelea kuchukua tahadhari  kwa kuepuka kuingia kwenye mitego ya matapeli , sambamba nakutoa taarifa ya vitendo hivyo Ili wachukue hatua mara moja.



Post a Comment

0 Comments