Wachimbaji na wachenjuaji wadogo wa
madini ya dhahamu
Mtaa wa Mgusu mjini Geita
Wachimbaji
na wachenjuaji wa madini ya dhahabu
katika Mtaa wa Mgusu Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita wametakiwa
kuzingatia usafi wa mazingira ili kuepukana na Magonjwa ya Mlipuko wakati huu
wa msimu wa mvua.
Akizungumza
na kituo hiki Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafi kutoka katika Halmashauri ya
Mji wa Geita Ndg. Aloyce Mtayuga amewataka wananchi katika eneo hilo kuwa
mstari wa mbele katika kuahakikisha Usafi unafanyika kila mara bila
kushurutishwa.
Mtayuga
amesema zoezi la usafi katika baadhi ya maeneo imekuwa ni changamoto hali
ambayo imekuwa ikiwapa Muda mwingi wa kuzungukia Maeneo yenye changamoto
hususani katika migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.
Kaimu
Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Benson Kinaamila ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wakazi
wa eneo hilo kuendelea kuzingatia usafi hususani katika maeneo yao ya uchimbaji
na uchenjuaji wa madini ya dhahabu.
Baadhi
ya wakazi wa eneo hilo wamesema ukosefu wa sehemu maalumu ya kuhifadhi taka
ngumu ndiyo changamoto kwao yakushindwa
kuhili masuala ya usafi wa mazingira kwakuwa shughuli zao zilazalisha taka kwa
wingi.
0 Comments