TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WANANCHI MKOANI GEITA WAMESHAURIWA KUENDELEA KUJIUNGA KATIKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

 

Meneja wa NHIF Mkoa wa Geita Elias Odhiambo

Wananchi Mkoani Geita wameshauriwa kuendelea kujiunga katika Mfuko wa taifa wa bima ya Afya NHIF kwakuwa huduma za mfuko huo zimeendelea kuboreshwa ili kuwafikia watu wote.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoani Geita Bw Elias Odhiambo katika kikao na waratibu wa mfuko huo mkoani Geita kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari waja  Geita mjini nakusema kuwa mfuko huo ulianzisha utaratibu wa kuwa karibu na wananchi kwa kusogeza huduma hizo hadi ngazi za wilaya.

Wadau wa mfuko wa NHIF mkoani Geita wakiwa katika kikao

Bw Odhiambo amesema  kila mtanzania anaweza kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya awe ni mwajiriwa , amejiajiri mwenyewe, mtu binafsi , motto mwenye umri chini ya miaka 18,wakulima,wachimbaji wadogo wa madini na makundi yote katika jamii.

Mratibu wa NHIF wilayani Chato Dkt Harriety Majaliwa

Amesema lengo la kikao hicho nikuwajengea uwezo waratibu wa mfuko  huo  kutoka wilaya  zote za mkoa wa Geita ili waweze kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kuona umuhimu wa kujiunga kwenye mfuko huo.

Kwa upande wao baadhi ya waratibu wa NHIF walioshiriki katika kikao hicho mbali nakuahidi kuendelelea kutoa elimu,wamewashauri wananchi Mkoani Geita kuchangamkia fursa  ya kujiunga  na mfuko huo kwani ugonjwa hautoi taarifa.

Post a Comment

0 Comments