TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WANAUME WANAOFANYIWA VITENDO VYA UKATILI NCHINI WATAKIWA KUTOONA AIBU KURIPOTI VITENDO HIVYO

 

Baadhi ya wanaume wanaofanyiwa  vitendo vya ukatili na wake zao nchini wameshauriwa kuendelea  kuripoti  vitendo hivyo kwa mamlaka husika ili waweze kusaidiwa.

Rai hiyo imetolewa na katibu Mkuu wa Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania Bw Antony Solo wakati akizungumza na Storm Fm nakusema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili nakushindwa kuripoti vitendo hivyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuona aibu.

Bw Solo amesema kwa utafiti uliofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu mwaka 2012 katika mikoa mitatu ya Tanzania bara na mmoja kutoka zanzibari, mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya kusini ikiwemo mkoa wa Lindi ndio inaongoza kwa wanaume wengi kufanyiwa vitendo vya ukatili, nakuwataka wanaume wote nchini wanaofanyiwa vitendo hivyo kuendelea kujitokeza ili waweze kusaidiwa.

Mmoja wa wanaume aliewahi kufanyiwa ukatili na mwenzi wake nakujitokeza kuripoti tukio hilo kwa mamlaka husika  bila kutaja  majina wala makazi yake ameiomba serikali kuendelea kukemea vitendo hivyo ikiwemo kutoa maamuzi sawa pale mwanaume anapokwenda kulalamika.


Post a Comment

0 Comments