Kaimu Ofisa Afya na Mazingira wa Halmashauri
ya Wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita Bw Ntiliyo Ezekiel
Wawekezaji
nchini wameshauriwa kuwekeza katika miradi ya usafi wa mazingira ili kuweza kuepukana
na uchafuzi wa mazingira ambao unaweza kupelekea mlipuko wa Magonjwa yatokanayo
na uchafuzi wa mazingira.
Wito
huo umetolewa na kaimu Ofisa Afya na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nyang'hwale mkoani Geita Ntiliyo Ezekiel wakati
akiongea na kituo hiki, Katika kampeni ya usafi wa mazingira katika mamlaka ya
mji mdogo wa Kharumwa na maeneo mengine ya wilaya hiyo.
Ezekiel
ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wawekezaji kuwekeza katika miradi ya usafi
wa mazingira, kwani kwa kufanya hivyo itawanufaisha kiuchumi na kuisaidia
serikali kuokoa fedha inayotumika kugharamia matibabu na kununua vifaa tiba ili
kudhibiti Magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kichocho.
Kwa
mjibu wa ofisa huyo, amekieleza chombo hiki cha habari kuwa, Tafiti za
wataalamu wa maswala ya Afya zinaonesa kuwa, Kila ikiwekezwa Dola Moja katika
mradi wa usafi wa Mazingira, huokoa zaidi ya Dola Kumi ambazo zingeenda katika
manunuzi ya Dawa na vifaa Tiba kwa ajili ya kugharamia matibabu ya Magonjwa
yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.
Ameendelea
kufafanua kuwa katika wilaya hiyo wawekezaji wengi huwekeza katika sekta ya
madini sekta ambayo imetajwa kuwa ni kichocheo kikubwa Cha uchafuzi wa vyanzo
vya maji na mazingira kwa ujumla.
Mmoja
Kati ya wekezaji katika Sekta ya Madini na mwanasiasa Nguri wilayani humo,
ambaye hakupenda jina lake litajwe, amekiambia chombo hiki Cha habari kuwa,
wanashindwa kutekeleza matakwa ya kisheria ya utunzaji wa mazingira kutokana na
mitaji midogo waliyonayo hivyo kushidwa kujenga miundombinu imara ya kulinda na
kuhifadhia taka.
Ameongeza
kuwa katika swala la kuwekeza katika miradi ya uhifadhi wa mazingira, ni fulsa
nzuri, hivyo amewataka wawekezaji mbalimbali kuitazama katika jicho pevu, ili
jamii iweze kunufaika kupitia uwekezaji huo ambao unatanjwa kuwa na tija kwa
makundi yote.
Baadhi
ya wananchi wa wilaya hiyo akiwemo Samson kinuno ameeleza kuwa, shughuli
za uchenjuaji wa dhahabu ni kichocheo kikubwa cha uchafunzi wa vyanzo vya maji,
hali ambayo inaweza kusababisha Magonjwa Nyemelezi yanayoweza kupelekea mlipuko
wa Magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo salama.
Mwananchi
huyo aliendelea kujipambanua kuwa Wakazi wengi wa wilaya hiyo wanategemea maji
ya visima vya asili na Yale ya ziwa Viktoria hivyo kuendelea kufanya uchafuzi
katika vyanzo vidogo vinavyopokea maji kutoka chanzo kikubwa ambacho ni ziwa
Vikitoria, inaweza kuhatarisha afya za watu wengi hivyo kuomba serikali kuchukua
hatua ili kudhibiti mazingira.
0 Comments