Waziri wa Maji Mhe, Jumaa Aweso amewasimamisha kazi
meneja na kaimu meneja wa huduma za maji mjini na vijijini RUWASA wilaya ya
Geita kwa kushindwa kusimamia vizuri mradi wa maji wa Nyakagomba na Chankorongo
uliyopo wilayani humo.
Akiwa
katika ziara ya siku moja ya kukagua
miradi hiyo wilayani Geita Waziri Aweso
amewasimamisha kazi Meneja wa Huduma za maji mjini na vijijini RUWASA wilayani
Geita Sani Sonda na kaimu wake Omega Agustino kwa kushindwa kusimamia miradi
hiyo vizuri.
Mbunge wa jimbo la Busanda wilayani Geita Tumain Magesa amesema mradi wa Nyakagomba umetumia zaidi ya shilingi milioni 600 na ulianza kutekelezwa mwaka 2009 bila mafanikio yoyote mpaka sasa.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandis Robert Gabriel amesikitishwa na utendaji mbovu wa
wahandis hao nakutumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wengine kuwa wakati
huu ni wakati wa kazi.
0 Comments