Makamu Rais wa kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML) Mhe. Saimon Shayo akizungumzia mchango wa sekta ya madini mkoani Geita amesema kwa kipindi cha miaka mitatu mgodi wa GGML umechangia zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa lengo la kusaidia jamii katika shughuli za maendeleo.
"Tunaishukuru
serikali kwa kuendelea kuleta
sheria mpya ambazo
ziemeendelea kuwatambua wazawa,
lakini kipekee niishukuru
serikali kwa namna ambavyo
imeendelea kutambua mchango
wa kampuni ya GGML katika suala la kurejesha faida wanayopata kwa jamii inayozunguka mgodi huo (CSR)" alisema Simon Shayo Makamu wa Rais wa kampuni ya Geita Gold Mine Limited - GGML). Makamu wa Rais wa mgodi GGML ameishukuru
serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kwa utekelezaji wa sheria mpya zilizofanyiwa marekebisho mwaka
2017 zinazo husu washiriki wazawa katika sekta ya madini (Local content).
Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMETA) Mhe.John Bina akitoa salaam za wachimbji wadogo alisema kuwa wachimbaji wataendelea kulipa kodi za serikali huku akiiomba serikali kuweka msukumo kwenye taasisi za kifedha ziweze kuwakopesha mikopo ya masharti nafuu.
0 Comments