TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

MGODI WA BUCKREEF WADHAMIRIA KUWASAIDIA WANANCHI GEITA

 

Meneja rasilimali watu mgodi wa Buckreef Amelda Msuya akitoa maelezo kwa mbunge wa jimbo la Geita Mjni Costantine Kanyasu aliyevaa koti.

Mgodi wa Buckreef uliopo katika kijiji cha Mnekezi kata ya Kaseme Wilaya ya  Geita umetenga zaidi ya shilingi milioni 321 ambazo ni fedha za uwajibikaji wa kampuni katika jamii (Corporate Social Responsibility-CSR) kwa kipindi cha mwaka 2021/2022.

Meneja rasilimali watu wa Mgodi huo Amelda Msuya amesema hayo wakati Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Mhe. Costantine John Kanyasu alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye uwanja wa maonesho ya teknolojia ya uchimbaji madini ya dhahabu uliopo eneo la uwekezaji (Export Processing Zone-EPZ) mjini Geita .

Meneja huyo amesema kuwa Mgodi huo una ubia kati ya serikali na mwekezaji TANZAM 2006 ambapo serikali inachukua 45% na mwekezaji huyo 55% hivyo kutokana na mgodi kutambua na kuthamini jamii inayowazunguka mgodi huo umetenga fedha hiyo kwa ajili wa uwajibikaji katika jamii.

Alisema mbali na kutenga fedha hiyo Mgodi huo umetumia zaidi ya shiligi milioni 32 kutoa msaada wa madawati na kukarabati miundombinu ya elimu katika shule za Tembo ,Kaseme Mkoani humo.

"Lengo la Mgodi ni kuhakikisha uchumi wa Mkoa wa Geita unapaa na jamii kunufaika na uwepo mgodi wetu"  ,alisema Meneja Msuya .


Meneja wa Benki NBC tawi la Geita Hilda Bwimba akitoa maelezo kwa mbuge wa jimbo la Geita Mjini Costantine Kanyasu alipotembelea kwenye banda hilo

Mbunge Kanyasu akiwa katika banda la Tume ya Madini alihoji uchelewaji wa leseni za uchimbaji madini ambapo mtalaamu tume ya madini Achar Kashakar alisema tume ya madini imeboresha mfumo wa utoaji leseni za uchimbaji ambapo waombaji kwa sasa wanaomba na kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

Mbunge huyo mara baada ya kutembelea mabanda katika uwanja huo alisema maonesho hayo yanaonesha sura ya kitaifa na hivyo kuwataka wachimbaji wa madini ya dhahabu kujitokeza katika maonesho hayo ili kuweza kujifunza namna bora na ya kisasa ya uchimbaji madini.

Post a Comment

0 Comments