TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WAZIRI MKUU AMEAGIZA BENKI KUWAKOPESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika viwanja vya EPZA  kwenye maonesho ya nne ya teknolojia na  uwekezaji kwenye sekta ya madini mkoani Geita.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza kwenye maonesho ya nne ya teknolojia na uwekezaji  katika sekta ya madini mkoani  Geita.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ameagiza taasisi za fedha hususan benki kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwakopesha mikopo au vifaa vya uchimbaji  madini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akifungua rasmi Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye sekta ya madini  eneo la uwekezaji  EPZA Mkoani Geita huku akisema kuwa sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na kuchangia kwenye pato la Taifa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kwenye moja ya mabanda baada ya kuwasili katika viwanja vya EPZA  kwenye maonesho ya nne ya teknolojia  na uwekezaji  kwenye sekta ya madini mjini Geita.

Amesema taasisi za kifedha zimepewa dhamana ya kufanya shughuli zao na zinapaswa kuwasaidia wachimbaji kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu au vifaa na mitambo ya uchimbaji ili waondokane na kutumia dhana duni.

"Benki ya Taifa ya Biashara pamoja na taasisi zingine za kifedha zimeanza kuwa kopesha wachimbaji, taasisi za fedha wakopesheni fedha wachimbaji mikopo ya mashariti au vifaa vya uchimbaji na mitambo waachane na kutumia dhana duni", alisema Wazairi Mkuu.

Aidha mkrugenzi kitengo cha biashara kutoka benki ya taifa ya biashara NBC Elvis Ndunguru alisema kuwa Benki hiyo imeanza kutoa mikopo kwa vikundi vya wachimbaji mtu mmoja mmoja pamoja na watoa huduma migodini.
"Tumeanza utaratibu kuwapatia elimu wachimbaji wadogo na kuwakopesha wachimbaji wadogo kwa vikundi vya wachimbaji pamoja na mtu mmoja mmoja na baadae kuwakopesha mitambo kwa kutumia leseni zao kama dhamana", alisema Elvis.

Post a Comment

0 Comments