TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WILAYA YA NYANG’HWALE YAFANYA UCHAGUZI WA MADIWANI VITI MAALUMU KWA UWAZI NA USAWA

Na Editha Edward-Geita;

Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyang’hwale  Hamisi Tsaxara amewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa umoja wa wanawake Tanzania UWT wilayani humo kwa utulivu na umakini waliouonyesha katika uchaguzi wa kuwapata madiwani viti maalumu.

Hamis ambae ndie alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo alisema hayo mara baada ya kusoma matokeo ya uchanguzi huo ambapo alisema kuwa wilaya hiyo inakata 15 na tarafa 4.

 “Kama tulivyo sema mwanzo  hizi ni kura za maoni baada ya hapa kuna mchakato wa vikao , waliopiga kura katika tarafa ya Bukwimba wagombea walikuwa wawili, wajumbe waliopiga kura ni 862, kura zilizo haribika 23, kura halali 839 ambapo Magreth James Petro amepata kura 186 na Ester Mabura Sebastian amepata kura 653” alisema Hamisi.


Picha: Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyang’hwale  Hamisi Tsaxara

Katibu huyo alisema kuwa tarafa ya Msalala  wagombea walikuwa 4 na wajumbe waliopiga kura ni 860, kati ya kura 860 kura zilizoharibika ni 18, na kura halali ni 842. Matokeo Chausiku Masanja  Katoto kura 144, Bernadeta Aloyce kura 149, Salome Method Gwanchele  kura 216 na Grace  Lukasi Mavuno 332 na tarafa ya Nyang’hwale waliopiga kura  862 zilizo haribika ni 6, kura halali  856; matokeo Hongera Ibrahimu Luchemba alipata kura 84, Laulensia Jakobo Tome alipata kura 272 na Agnes Matibu Mashimi alipata kura 500.

Tarafa ya  Nyijundu waliogombea ni wawili na kura  zilizo pigwa ni 833 kura  zilizo haribika ni 5, kura halali 828; matokeo Herena Mahona Shija alipata kura 361  na Stella Slivanus Ndenge alipata kura 467;  wagombea mmoja mmjoja kila tarafa walioongoza kwa kura ndio watakao kuwa wawaklishi.

Kwa tarafa zote nne washindi  ni Ester Mabula Sebastian kutoka tarafa ya Bukwimba,  Grace Lukas Mavuno kutoka tarafa ya Msalala, Agnes  Matibu Mashimu kutoka tarafa ya Nyang’hwale, Stella slvanus Ndege kutoka tarafa ya Nyijudu na mtu watano ni Herena Mahona Shija uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Malala sekondari.


Picha: Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyang’hwale Happines Isack John 


          Picha: Katibu wa UWT Wilaya ya Nyang’hwale Bahati Kojogo 


Picha: Wajumbe wa mkutano wa UWT Wilaya ya Nyang’hwale wakiwa katika ukumbi wa uchaguzi wa madiwani viti maalumu.


Post a Comment

0 Comments