TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

WACHIMBAJI WASHIRIKIANE KUANZISHA BENKI YA MADINI GEITA



Pichani katikati ni Mhe.Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akiwa katika picha ya pamoja   na  baadhi ya wafanyakazi wa GGML (wenye T-shirts nyeupe) alipotembelea banda la Geita Gold Mine Limited -GGML kwenye maonesho,  kushoto kwake ni Mhe. Alhaji Kalidushi (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita) na wakwanza upande wa kulia ni Joseph Mangilima (Manager: Community Affairs-GGML) 



Mhe.Col (rtd).Ngemela Lubinga amesema ubora wa Mkoa wa Geita ni GGML, nakusema kuwa teknolojia inaenda kasi sana hivyo ingekuwa vyema kuanzisha benki ya Madini Mkoani Geita kwa lengo la Kuboresha Sekta ya Madini katika Uwekezaji wa kifedha, kupata mikopo wachimbaji wadogo na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Geita na Tanzania. 

“Wachimabji wote wa Madini Mkoani Geita waweke ushirikiano Mkubwa katika kuendeleza uchimbaji wa Madini hata katika kuanzisha Benki ya Madini kwa lengo la kuweka uwiano wa wachimbaji wadogo kupata nafasi ya kukopeshwa fedha kwenye benki hiyo ili kuendeleza uchumi” Mhe. Ngelema Lubinga amesisitiza.

Pichani akipokea zawadi ya mwavuli ni Mhe.Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akiwa katika picha ya pamoja  kwenye banda la  GGML  alipotembelea banda hilo kwenye maonesho,  kushoto kwake ni Mhe. Alhaji Kalidushi (Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita) 

Mhe.Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) amesema kuwa Mgodiwa GGML ni Mgodi unao fahamika  sana kwa kutetea na kuboresha mazingira ya uwepo wa uchimbaji wa kisasa wenye teknolojia ya hali ya juu na kuwaomba GGML waendelee kubuni na kutumia teknolojia za kisasa zaidi huku wakitoa semina elekezi kwa wachimbaji wadogo nao kuweza kujifunza kutumia teknolojia za kisasa katika uchimaji madini ili kuinua uchumi wa  Geita na Tanzania kwa Ujumla kupitia sekta ya madini.


Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akiwa katika banda la Wizara ya Madini alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho uwanja wa EPZA mjini Geita  leo 25/9/2021

Vilevile, Mhe.Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) amefurahishwa na jitihada kubwa sana za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za kuwa na banda la maonesho kwani inarahisisha kwa Chama kukuza wingo mpana wa kupata wanachama wapya na kuleta chachu ya kutekeleza shughuli za maendeleo kwa kufuta mwongozo wa Ilani ya Chama Cha Mpainduzi na serikali ya Chama Cha Mapinduzi katika Mkoa Wa Geita na Tanzania kwa Ujumla.

Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akiwa katika banda la CCM alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho uwanja wa EPZA mjini Geita  

Ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa  kuruhusu uwepo wa banda la Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kutoa huduma za kwa wananchi kwa kipindi chote cha maonesho ya Teknolojia na  uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akiwa katika banda la Mkuu wa Mkoa Geita alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho uwanja wa EPZA mjini Geita  Septemba 25,2021

 

Col (rtd).Ngemela Lubinga (Katibu NEC, Secretariat and Foreign Relations na Mlezi Mkoa wa Geita) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkuu wa Mkoa Geita alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho uwanja wa EPZA mjini Geita  Septemba 25, 2021



Post a Comment

0 Comments