WARATIBU wa Klabu za Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kuongeza jitihada za kufuatilia matukio ya ukiukwaji wa haki za binaadam dhidi ya waandishi wa habari kwani wao ni watetezi wa haki za binadamu na wamefundishwa kutoa taarifa juu ya matukio na vitendo vya ukiukwaji haki za binadamu kwa waandishi ikiwemo kunyimwa haki ya kupata taarifa kwaajili ya kuchukuliwa hatua.
Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu hao jana Jijini Dodoma, Ofisa Programu Mafunzo, Utafiti na Machapisho kutoka Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Victor Maleko amesema waandishi wa habari wamekuwa wakikabiliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kukwamisha utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Maleko amesema ili kufanikisha zoezi hilo UTPC imekuwa ikitoa mafunzo na midahalo mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari ikiwemo waratibu kujengewa uwezo wa kufuatilia madhila dhidi ya waandishi wa habari nchini Tanzania.
Pichani ni Waratibu wa Klabu za Waandishi wa habari nchini Tanzania wakifuatilia kwa ukaribu zaidi mkufunzi ambae pia ni wakili Bw. Jones Sendodo wakati akitoa mada mahususi kuhusu sheria za kitaifa na kimataifa juu ya haki za binadamu na haki za waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kukusanya, kuchakata, na kutoa habari. |
Akiwasilisha mada kuhusu uhuru wa kujieleza na akitumia uzoefu wake Wakili John Sendodo amesema ili kuweza kutambua haki za msingi za binadamu ni vyema kujua haki za kimataifa na namna nchi zingine zimekuwa zikitekeleza haki hizo.
Pichani ni Waratibu wa Klabu za Waandishi wa habari nchini Tanzania wakifuatilia kwa ukaribu zaidi mkufunzi ambae pia ni wakili Bw. Jones Sendodo wakati akitoa mada mahususi kuhusu sheria za kitaifa na kimataifa juu ya haki za binadamu na haki za waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kukusanya, kuchakata, na kutoa habari. |
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la IMS Zimbabwe, Rashweat Mukundu ametoa uzoefu wake kuhusu madhila yanayotokea Zimbabwe na kuwataka waratibu hao kuwa makini wakati wa kuchambua madhila hayo kwa kuwa wanaoyafanya na wao hutumia akili nyingi sana.
“Nchini Zimbabwe waandishi wa habari wanafanyiwa sana madhila lakini kama hauko makini unaweza usibaini ukweli wa tukio lililotokea, hivyo mbinu mbalimbali zinahitajika ili kuweza kubaini,”amesema.
Kwenye picha ni Bw. Seif Mangwangi Mwenyekiti wa Waratibu wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania ambae pia ndiye Mratibu wa Arusha Press Club-APC (kulia) akitafakari mafunzo ya haki za binadamu hususan waandishi wa habari na kushoto kwake ni Mr. Hafigwa mratibu wa Morogoro Press Club. |
Pia amewataka waratibu kuripoti haraka matukio ya madhili pindi yanapotokea ili kurahisisha upatikanaji wa mwandishi aliyetendewa tukio husika lakini pia kufanya uchambuzi wa kina na kubaini ukweli ili kuepuka mgogoro usiokuwa wa lazima na mamlaka za kiserikali.
Katika picha ni Waratibu wa Klabu za Waandishi wa Habari wa klabu ya Kigoma Press Club Dianna Rubanguka (kushoto), na Mwajuma Kitwana mratibu wa Mtwara Press Club (kulia)wakiwa kwenye mafunzo ya namna ya kuripoti madhira yanayo wakumba waandishi wa habari Tanzania. |
0 Comments