Na Mwandishi Wetu, Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kujiletea maendeleo, " Nitoe wito kwenu kila mmoja afanye kazi kama vile atakufa leo ili uhuru huu uendelee kuleta maana na kuonesha thamani na maendeleo hivyo kila mmoja afanye kazi kwa kujituma na kwa bidii kwani uchumi haukui kwa kulala usingizi" amesema.
Amesema hayo leo tarehe 8 Disemba ,2021 wakati akiwaongoza wananchi wa mkoa wa Geita kwenye maadhimiosho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa GEDECO mjini Geita ambapo pia amewataka viongozi wa dini katika mkoa huo kuwaunganisha watanzania ili kulinda umoja na mshikamano uliopo nchini kama tunu ya taifa ili kuenzi amani na mshikamano uliopo nchini.
vile vile Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule amesema baada ya Baba wa Taifa viongozi waliofuata waliendelea kuboresha miundo mbinu ya bara bara na miundombinu nyingine za kutolea huduma za afya kwa wananchi kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa.
Hata hivyo amewataka wananchi wake pamoja na kufanya kazi kwa bidii wachangamkie fursa ya kupata chanjo kwa hiari ya UVIKO 19 ili kujikinga na maradhi hayo ambayo hivi sasa tupo kwenye wimbi la nne la ugonjwa huo.
Picha ya wananchi waliohudhuria hafla ya maadhimiosho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa GEDECO mjini Geita 8/12/2021 |
Picha ya wananchi waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa GEDECO mjini Geita 8/12/2021 |
0 Comments