Na Mwandishi Wetu, Geita
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) imepokea hati ya kutambua ushiriki wake kwenye maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yaliyoanza tarehe 16 hadi 26 Septemba 2021 katika uwanja wa kituo cha uwekezaji Bombambili mjini Geita kutoka kwa Ofisa habari wa Mkoa wa Geita Paul Zahoro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary S. Senyamule leo tarehe 08/12/2021.
Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yaliasisiwa rasmi katika Mkoa wa Geita kwa mara ya kwanza mwaka 2018, na yamekuwa yakifanyika kila mwaka huku Geita Press Club-GPC ikishiriki kikamilifu kwenye maonesho hayo kwa miaka yote 2018, 2019, 2020 na 2021 kwa awamu ya nne.
Marabaada ya kupokea hati hiyo ya kutambua ushiriki wa GPC kwenye maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini kutoka kwa Ofisa habari wa Mkoa wa Geita Bw.Paul Zahoro aliekabidhi hati hiyo kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Geita Bw. Renatus B.D.Masuguliko, ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kuonesha kwa vitendo kutambua ushiriki wa Klabu ya Waandishi wa habari kwenye maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini, na kuahidi waandishi wa habari kuendelea kutoa ushirikiano katika shughuli mbali mbali za mkoa huo wa Geita.
0 Comments