Mwonekano wa barabara na baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza wakishangilia taa za barabarani.
Na Anna Ruhasha, Mwanza.
Wananchi wilayani Sengerema mkoani mwanza wameiponge serikali ya awamu ya sita kwa kuweka taa za barabarani ambapo kilikuwa kilio chao cha muda mrefu husasani kwa wafanyabiashara , mama ntilie na bodaboda.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Vaireth Ndembeto na Joshua Mabula wamesema kuwa kwa sasa wilaya ya Sengerema imegeuka kuwa Ulaya ndogo huku wakifanyabishara zao nyakati za usiku bila bugudha.
Sambamba na Pongezi hizo kwa serikali y awamu ya sita ya Mh Rais Samia Suluu Hasani pia wamempongeza mbunge wa jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu kusimamia vyema maendeleo ya Sengerema kuhakisha anatekeleza ahadi alizoziahidi wakati akiomba ridhaa ya kuongoza wananchi wa Sengerema mkoani mwanza.
“Kwakweli Mh Tabasamu anafanyakazi na ukiangalia tangu aingie madarakani asilimia kubwa yale aliyotuahidi ametekeleza ,tunamshukuru pia”wamesema.
Hata hivyo taa hizo mpaka sasa zimefungwa zaidi ya kilometa mbili huku zikiendelea kufungwa kwa mji wa Sengerema.
Mwisho
0 Comments