TANGAZA NASI: geitapressclub@gmail.com

BWAWA LA TOPE KALI LA PASUKA

Muonekano wa mazingira ya mashamba ya wananchi yalivyoathiriwa na Tope kutoka Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond wa Mwadui Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.

 Na Paul Kayanda, Shinyanga

KAYA 19 za Vijiji vitatatu vya Iyenze, Mwaholo na Kabondo Kata ya Mwadui vinavyozunguka Mgodi wa Alimasi wa Williamson Diamond Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga vimedaiwa kuathirika zaidi baada ya kuzingilwa na Maji yenye tope kali kutoka mgodini hapo kwa madai ya Bwawa la kuhifadhia tope mgodini kupasuka.

Baada ya kingo za bwawa hilo la Mgodi huo kupasuka Ekari kadhaa za mashamba ya wananchi pamoja na nyumba zimeathiriwa na Tope kali hali ambayo imesababisha hasara ya vyakula na visima vya maji kufunikwa na Tope hilo.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti na Waandishi wa Habari Jigo Tenga, Maria Juma pamoja na Ester Thomas Wameiomba Serikali kupitia kamati ya maafa ya Mkoa wa Shinyanga ichukue hatua za haraka kutatua changamoto hiyo kwani baadhi yao wamepoteza mifugo 15 ya Ng’ombe pamoja na kukosa makazi ya kuishi.

Muonekano wa mazingira ya mashamba ya wananchi yalivyoathiriwa na Tope kutoka Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond wa Mwadui Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.

Tope limenivamia kwenye shamba langu,hili ni jambo geni kwangu sijaliona tangu kuzaliwa kwa mantiki hii sina sehemu ya kulima, na kuna watu wengine wamepotea mpaka sasa hatujawaona,” alisema Jigo Tenga.

Hata hivyo kwa upande wake Maria Juma akizungumzia tope hilo amesema kuwa kwa sasa mashamba yake yamejaa tope kote anakotegemea kulima na kwamba hata mifugo nazo zimedidimia kwenye tope, ng’ombe 15 mbuzi sita hazionekani mpaka sasa.

Hapa nilipo nafamilia ya Watoto watano, hatujui tunapoenda, na tutalala wapi leo, Maisha ndo haya yamekuwa magumu kwa maana hali ya hapa inatatanisha maana hilo tope linaweza kuingia ndani likasababisha vifo mimi na Watoto wangu nimeona tu nitoke nijibanze mahali popote sina la kufanya mie,”amesema Esther Thomas.

Aidha wanaomba msaada kwa wadau mbalimbali watakaoguswa na hali yao ili wapate kujihifadhi na kupata chakula wakati serikali itakaposikia kilio hiki na Kwenda kuwasaidia.

Hata hivyo leo Novemba 8, 2022 uongozi wa Mgodi huo kupitia afisa mahusiano wake Leonard Mihayo alipotakiwa kuzungumzia ajali hiyo alidai kuwa msemaji wa tukio hilo kwa sasa ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sofia Mjema.

Mwisho


Post a Comment

0 Comments